WATUHUMIWA wanne kati yao wakiwemo watatu wa kesi ya mauaji wamevunja mahabusu ya kituo cha kati (Central) Mbeya na kutoroka.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alilosema limetokea usiku wa kuamkia jana machi 22 majira ya usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa hivi.
Amesema kati ya watuhmiwa hao watatu ambao hakuwataja majina wanakabiliwa na kesi moja ya mauaji na mmoja aliyemtaja kwa jina la Fadhil Mwaiteleke(27) mkazi wa Ilomba jijini Mbeya anakabiliwa na tuhuma za wizi wa betri tatu za gari.
Amesema kwa pamoja watuhumiwa hao waliokuwa katika moja ya vyumba vipya vilivyoongezwa katika upanuzi na uboreshaji wa mahabusu ya kituo cha kati uliofanyika hivi karibuni walifungulia maji na kulainisha ukuta kwa kuumwagia maji kabla hawajatumia vipande viwili vya nondo kuchimba ukuta huo na kutoroka.
Amesema askari waliokuwa zamu ya usiku katika chumba cha mapokezi ya mashitaka kama kawaida yao ya kukagua mahabusu kila baada ya saa moja walifika katika chumba hicho na kusikia maji yakimwagika kwa wingi hali iliyoonesha bomba lilikuwa limeachwa wazi.
Baada ya kuchunguza walibaini kuwa mahabusu wanne waliokuwamo walikuwa wametoroka kupitia tundu lililochimbwa ukutani na kukuta vipande viwili vya nondo vilivyoachwa vinavyosadikiwa kuwa kuna mtu aliyeviingiza humo kutoka upande wan je kupitia matundu madogo yaliyopo upande wa juu wa ukuta
Kamanda huyo amefafanua kuwa baada ya askari hao kubaini kutoroka kwa mahabusu walitoa taarifa kwa vyombo vingine vya usalama na kwa ushirikiano wa pamoja usiku huo wakafanikiwa mahabusu Mwaiteleka akiwa katika jitihada za kutokomea mbali zaidi.
Kwa hisani ya Joachim Nyambo
|
No comments:
Post a Comment