Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 2, 2011

WANANDOA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO - MBEYA



Na mwandishi wetu.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili ambao ni wanandoa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wao Nuru Mzumbwe mwenye umri wa miaka 10 mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Idiwili iliyopo wilayani Mbozi mkoani Mbeya

Waliokamtwa kuhusika na tukio hilo ni mama mzazi Diana Mwampashi mwenye umri wa miaka 20 na Stephano Mzumbwe mwenye umri wa miaka 38 wote wakazi wa kijiji cha idiwili.

Inadaiwa kuwa Bi.Diana ambaye ni mama mzazi wa Nuru alimpa sumu mwanae ambayo ilikuwa imewekwa kwenye chai na andazi kutokana kile kilichoelezwa kuwa mama huyo alikuwa akimtuhumu mumewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mdogo wa mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Sesy Mwampashi. 

Tukio hilo limetokea October 29 katika kijiji cha Idiwili majira ya saa saba za mchana wakati  mtoto huyo alikuwa akipata chakula cha mchana.

Kutokana na tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa hao kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

No comments: