Mwenyekiti wa chama cha demokrasi na maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akiwasili kwenye Ofisi za Jeshi la Polisi Mkoani Arusha leo asubuhi kwa ajili ya kujisalimisha kufuatiwa kusakwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kuvunja sheria.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiingia katika ofisi za mkoa za Jeshi la Polisi mkoni Arusha leo,aliyevaa nguo nyeusi ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Joyce Mukya akiwa amemsindikiza mwenyekiti wao kujisalimisha Polisi.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiwa anatafakari jambo ndani ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha leo.
Mkuu wa Operation wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha,Saimon Pilo (kulia) akiwa amempokea Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe (katikati) katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanya nae Mazungumzo,wakati Mwenyekiti huyo alipofika Kituoni hapo Kujisalimisha leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment