Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 9, 2011

MAOFISA EWURA WAWASILI MKOANI MBEYA KUJADILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA KULIPIA HUDUMA YA MAJI.

Na mwandishi wetu
Maofisa wa mamlaka ya nishati na maji (EWURA) wamewasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kujadili namna ya kupunguza gharama ya kulipia huduma ya maji wilayani Rungwe baada ya wananchi wa wilaya hiyo kumuomba mkuu wa wilaya hiyo awasaidie kushusha gharama ya kulipia maji na kwamba gharama iliyopo hawana uwezo wa kuilipa.

Baada ya ombi hilo mkuu wa wilaya ya Rungwe Jackson Msome aliahidi kulifuatilia suala hilo ambapo mara baada ya viongozi hao wa EWURA kuwasili wamekutana na uongozi wa wilaya na mkoa ili kuangalia namna ya kukabiliana na suala hilo.

Wananchi wa wilaya hiyo walitishia kugoma kulipia gharama mpya za matumizi ya maji baada ya EWURA kupitisha mapendekezo ya kupanda kwa gharama za maji kwa asilimia 125.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Rungwe Jackson Msome amesema kuwa majadiliano kati ya Serikali na Ewura yamemalizika na kwamba kesho kutakuwa na mkutano wa wananchi ili kutoa mapendekezo ya gharama mpya za matumizi ya maji.

No comments: