Na mwandishi wetu
Wananchi waishio kandokando ya uwanja wa ndege jijini Mbeya wametakiwa kutokatisha katikati ya uwanja huo ili kuifanya njia ya kurukia ndege kuwa salama wakati wote.
Akizungumzia meneja wa uwanja huo Bwana Ezekiel Mwalutende amesema licha ya kutolewa kwa elimu na matangazo yanayohusiana na madhara yatokanayo na wananchi kukatisha uwanjani bado baadhi yao wamekuwa wakiendelea kukaidi agizo hilo.
Kwa upande wao wakazi wanaoishi karibu na uwanja huo wamesema sababu inayochangia wananchi wa eneo hilo kukatisha uwanjani hapo inatokana na maeneo yao kutokuwa na vyombo vya usafiri hali inayowapelekea kuchelewa kufika katika sehemu zao za kazi hasa zaidi kwa upande wa wafanyabiashara wa soko la Mwanjelwa Sido.
Hata hivyo inadaiwa kuwa baadhi ya walinzi uwanjani hapo wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa wananchi kukatisha kwenye uwanja huo kutokana na kutokuwa makini katika shughuli yao ya ulinzi.
No comments:
Post a Comment