Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 25, 2011

SAKATA LA BEI YA UNUNUZI WA GARI ZA KUZOLEA TAKA LA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA.

Gari la kuzolea taka la halmashauri ya jiji la Mbeya.(Picha na mtandao huu)
******
Na Gabriel Mbwille.
Mkaguzi mkuu wa Serikali kanda ya nyanda za juu kusini Mohamed Ramadhani amesema kuwa gari la kubeba taka lililonunuliwa na halimashauri ya jiji la Mbeya kwa shilingi milioni 300 linathamani ya shilingi milioni 20.

Akisoma taarifa hiyo ndani ya kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi mwishoni mwa wiki amesema kuwa gari hilo limetumika hivyo fedha stahiki ilitakiwa Jiji hilo litoe ni shilingi Milioni 20 lakini viongozi waliokuwepo waliidhinisha Shilingi Milioni 300.

Aidha katika hadidu rejea za Juni 19 mwaka huu za kikao cha Baraza la Madiwani waliazimia kumrejesha Jijini Mbeya aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji mwaka 2008, mweka hazina na Afisa ugavi wa kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye alialikwa katika kikao hicho alimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Idd kwa kuendelea kuziba mianya ya ubadhilifu katika Jiji hilo na kwamba Serikali itaendelea kumlinda.

No comments: