Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, amesema matatizo aliyokabiliana nayo katika uongozi wake ni ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya maofisa na watendaji kwa kuiba fedha benki.
Amesema iwapo hali hiyo haitaweza kudhibitiwa mapema ni wazi hata akitokea kiongozi wa aina yoyote itamuwia vigumu kuwafikishia maendeleo wananchi wake.
Mwakipesile ameyasema hayo wakati akizungumza katika hafla ya kumuaga na kumkaribisha Mkuu mpya wa mkoa, Abbas Kandoro, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini hapa.
Mkuu huyo wa mkoa mstaafu, ameongeza kuwa viongozi hao wanatakiwa kuwa kitu kimoja, kwani serikali kuu imekuwa inapeleka mamilioni ya fedha kwenye halmashauri nchini, lakini yamekuwa yanaibwa na watu wachache.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro ameahidi kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na Mwakipesile katika utawala wake.
No comments:
Post a Comment