Soko dogo la Uyole Jijini Mbeya Tanzania
*****
Na mwandishi wetu
Wafanyabiashara wa soko la Uyole Mbeya wameuomba uongozi wa halmashauri ya jiji kuboresha miundombinu ya soko ili kukabiliana na janga la moto pindi linapotokea pamoja na kuchimba mitaro ya kupitisha maji taka wakati wa masika.
Ombi hilo wamelitoa kufuati soko hilo kutokuwa na njia ya kupitisha magari ndani ya soko hali inayohatarisha usalama wa mali za wafanyabiashara hasa yanapotokea majanga ya moto.
Aidha mfanyabiashara Marko Sanga amesema endapo itashindikana kupanua barabara za soko hilo ni vyema umeme uliowekwa ukaondolewa na kuongeza kuwa ushuru wa shilingi elfu moja wanaotozwa ni mkubwa kiasi na hauendani na kipato chao.
Naye mkuu wa soko hilo Isaya John amesema kuwa wiki lijalo halmashauri ya jiji itanza kupanua barabara za soko hilo pamoja na ujenzi wa mitaro ili kuondoa kero wanawazokabiliana nazo na kuongeza kuwa suala la ushuru atalifuatilia kutokana na kwamba kila mfanyabiashara anatakiwa kutoa shilingi mia mbili kwa kila gunia la vitunguu na sio shilingi elfu moja kwa gunia kama inavyodaiwa.
No comments:
Post a Comment