Na Andrew Chale,
KUNDI la Uswaz Donta linaloundwa na wasanii wawili wanaoishi maisha ya mitaani, Hasan Issa ‘H. Genius’ na Gasper Mpepo ‘Kimwanya Mc’ wameomba wadau kuwapa tafu ya kuingia studio.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mapema leo jijini Dar es Salaam, Uswaz Donta ambao maskani yao, maeneo ya chuo cha usimamizi wa fedha ‘IFM’ ambapo wanajihusisha na uoshaji wa magari, walisema wametafutaa pesa kwa muda mrefu lakini walifanikiwa kupata laki moja na ishirini hata hivyo fedha hizo hazitoshi kuingia studio.
“Kwa muda mrefu tunasaka pesa hatuna kazi maalum zaidi ya kuosha magari sisi watoto wa mitaani na kipaji chetu ni sanaa na muziki hivyo tunaomba kupigwa tafu ilikuingia studio ilikufikisha ujumbe wetu kwa jamii” alisema H.Ginius.
Pia alisema kuwa, wana karibu nyimbo 12 ambazo zinatosha kufanya albm nzima ila kama atajitokeza mdhamini wa kuwapeleka studio wapo tayari kutoa hata nyimbo nne ambazo zimejaa ujumbe kwa jamii sambamba na kuburudisha.
.. “Tumeshaaongea na projuza Ulamaa wa studio ya Fish Club, amesema yupo tayari kututengezea nyimbo kwa kiasi cha laki tatu hivyo kwa mdau aliye tayari anaweza kuwasiliana nasi ilikuingia studio” alisema Kimwanya Mc.
Walizitaja nyimbo zao ambazo wapo tayari kuingia studio kuwa ni pamoja na ‘Naishi Kiimani’, ‘Hili ni fundisho’, ‘Wanabugi ramani’ na ‘Shule’ ambapo nyimbo hizo wamekuwa wakizifanyia mazoezi muda wote.
Aidha kundi ambao wote wamekulia mitaani huku wakiosha magari, wamesema wameamua bora kudunduliza kiasi cha fedha ili kuwawezesha kuingia studio na kufikisha ujumbe wao huo ili kilio chao kifike kwa jamii.
Pia waliendelea kusema kuwa, kwa mdau anaweza kuonana nao na kuwalipia kuingia studio yoyote ili kukidhi hadhima yao hiyo.
“Watoto wa mitaani tunakosa fursa nyingi ila vipaji vipo huku vingi na huu ni mwaka wa tatu tunatafuta pesa lakini tunakosa kama tungefanikiwa kwa sasa tungeshaingia studio kukamilisha nyimbo zetu hivyo ilani yetu tunaomba wadau kutupa tafu angalau kutualika kwenye shughuli mbalimbali kutoa burudani pamoja na matamasha ilikuonyesha uwezo wetu” walisema Uswaz Donta
Kwa atakayekuwa tayari anaweza kuwasiliana na Uswaz Donta lipitia namba yao ya simu ya mkononi; 0717149314 ama kupitia Andrew Chale, mwandishi na msimamizi wa kundi hilo;+255719076376,andrewchale@gmail.com///ama unaweza kuonana nao kijiweni kwao maeneo ya IFM, pembezoni mwa ukuta wa IFM na Makumbusho ya Taifa wakijishughulisha na uoshaji wa magari
No comments:
Post a Comment