Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 4, 2011

MAKAMU WA RAIS USO KWA USO NA MAALIM SEIF SABASABA BAADA YA KUZINDUA GS 1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Huduma Global Standard GS1 nchini Tanzania, ‘Mfumo wa utambuzi wa Bidhaa’Uliozinduliwa leo Julai 04, 2011 kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Dar es Salaa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi huduma mpya ya Mfumo wa Utambuzi wa Bidhaa Tanzania, (Global Standard 1 ), wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere leo Julai 04, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa leo Julai 04, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Biala, akisikiliza maelezo ya mjasiliamali, Angela John, kuhusu mashine ya Kusokota, wakati alipotembelea katika Banda la Sido kwenye Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Power Electronics & Controls Ltd, Kayungi Kayungi, kuhusu Mashine ndogo inayozalisha Umeme kwa kutumia maji, wakati alipotembelea Banda la Sido kwenye Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam
Picha na Muhidin Sufiani-OMR  

No comments: