Mkurugenzi wa Kampuni ya BenchMark Production, Madam Ritha Paulsen akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza uzinduzi rasmi wa mashindano ya Bongo Star Search 2011.kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe.
KAMPUNI ya BenchMark Production Ltd kwa kushirikiana na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager leo imezindua rasmi mashindano ya Bongo Star search 2011 yenye mwonekano wa kitofauti huku ikiwapa nafasi washiriki waliopita kuanzia mwaka 2006-2011, yenye kauli mbiu ya BSS 2ND CHANCE.
Shindano la BSS kwa Tanzania ndio shindano pekee la kusaka vipaji vya wanamuziki mbalimbali ambalo lilianza rasmi mwaka 2006, na kuweza kutoa nafasi kwa vijna wa kitanzania wenye vipaji vya kuimba muziki wa mahadhi mbalimbali na kuleta mafanikio makubwa kwa vijana hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya BenchMark Production, Madam Ritha Paulsen alisema tokea kuanzishwa mwaka 2006 mpaka 2010 BSS ilichukua ziara mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kutafuta Vipaji vya muziki na kupata washindi ambao wote waliweza kupata zawadi nono zilizoweza kuwasaidia kunyanyua mfumo wa maisha yao.
Aidha, kutokana na msimu wa mwaka huu kuwa wa kutoa nafasi ya pekee kwa washiriki wa nyuma, ni baada ya hivi karibuni , 2011,majaji wa BSS, kukaa chini na kupitia mikanda yote ya BSS zilizopita toka mwaka 2006 hadi 2010,na hatimaye kuwapata washiriki 30 ambao walikuwa na vipaji vizuri zaidi.
Kwa upande wake meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alishukuru kwa kampuni yake kuendelea kudhamini mashindano hayo ili kuendeleza vipaji vya watanzania ilikuwaletea maendeleo sambamba na kufurahia kinywaji bora cha Kilimanjaro Premium lager.
No comments:
Post a Comment