Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, May 11, 2011

Vodacom yatoa msaada wa madawati Shule ya Msingi Msigani iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam

Afisa Elimu  kata ya mbezi Veroni Mallya kushoto akishuhudia Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefula (kulia)akimkabidhi  Mwalimu Mkuu Zena Khakila wa  Shule ya Msingi Msigani iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4.  

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimsalimu mmoja wa wanafunzi wa  shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam mara baada ya kufika shuleni hapo kutoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4,anaeangalia kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zena Khakila.

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiweka nembo kwenye moja ya dawati kati ya 50 aliyotoa msaada kwa niaba ya kampuni yake katika  shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, madawati hayo yana  thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4. 

 
Mwanafunzi wa shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, Answary Waziri  akisoma nembo kwenye moja ya dawati kati ya 50  yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo.
 
Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakiangalia baadhi ya madawati  kati ya 50  yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakifurahia msaada wa madawati 50 waliyokalia  yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo,shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa madawati na madarasa.

No comments: