Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, May 6, 2011

kipindi kipya cha redio chazinduliwa kuelimisha watoto kuhusiana na ugonjwa wa malaria


BCC Program Manegar Waziri Nyoni akiongea na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kipindi cha redio cha watoto cha Patapata kitakachokua kinaelimisha na kuhamasisha kwa watoto juu ya ugonjwa wa Malaria wakati wa uzinduzi uliofanyika Kisarawe juzi.Kulia ni Mkuu wa Mradi (chief of part Commit)Robert Ainslie
Balozi wa watoto na mtayarishaji wa kipidi cha watoto cha radio One Edditha Mkwawa akiongea kwa niaba a watoto juu ya faida watakazo zipata katika kipindi hicho wakati wa uzinduzi wa kipindi cha redio cha watoto cha Patapata kitakachokua kinaelimisha na kuhamasisha kwa watoto juu ya ugonjwa wa Malaria uliofanyioka Kisarawe juzi.
Mkurugezi wa tiba Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Dr ,Margaret Everln Mhando (kushoto)akikata utepe wakati wa Uzinduzi kipindi cha redio cha watoto cha Patapata kitakachokua kinaelimisha na kuhamasisha kwa watoto juu ya ugonjwa wa Maralia wakati wa uzinduzi uliofanyika Kisarawe juzi.wengine ni BCC Program Manegar Waziri Nyoni na Mkuu wa Mradi (chief of part Commit)Robert Ainslie
Mkurugezi wa tiba Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Dr ,Margaret Everln Mhando (kushoto)akimkabidhi Mwl, wa Shule ya msingi Chanzige A, Victoria Nyangoro Radio itakayotumika kusikilizia kipindi cha Patapata wakati wa Uzinduzi kipindi cha redio cha watoto cha Patapata kitakachokua kinaelimisha na kuhamasisha kwa watoto juu ya ugonjwa wa Malaria wakati wa uzinduzi uliofanyika Kisarawe juzi.katikati ni Mkuu wa Mradi (chief of part Commit)Robert Ainslie
Mkurugezi wa tiba Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Dr ,Margaret Everln Mhando (kushoto)akimkabidhi Mwl, wa Shule ya msingi Chanzige B, Issack Eliah Radio itakayotumika kusikilizia kipindi cha Patapata wakati wa Uzinduzi kipindi cha redio cha watoto cha Patapata kitakachokua kinaelimisha na kuhamasisha kwa watoto juu ya ugonjwa wa Malaria wakati wa uzinduzi uliofanyika Kisarawe juzi.katikati ni Mkuu wa Mradi (chief of part Commit)Robert Ainslie
Balozi wa watoto na mtayarishaji wa kipidi cha watoto cha radio One Edditha Mkwawa akiwauliza maswali juu ya ugonjwa wa mMarelia watoto wa shule ya Chanzige A na B wakati wa uzinduzi wa kipindi cha redio cha watoto cha Patapata kitakachokua kinaelimisha na kuhamasisha kwa watoto juu ya ugonjwa wa Malaria uliofanyioka Kisarawe juzi.

===== ===== ===== ===== ====== ===== ===

Wazazi watakiwa kuwaruhusu watoto kujifunza.

Na Ripota Wetu, Kisarawe

WAZAZI nchini wametakiwa kutoa fursa kwa watoto wao kuweza kujifunza masuala mbalimbali yanayoathiri afya zao na pengine kuchangia kutokea kwa vifo visivyotarajiwa hususani kwa ugonjwa wa Malaria.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kipindi cha redio kitakachokuwa kinatoa elimu ya kujikinga na Malaria kwa watoto kwa shule za msingi Chanzige A na B Kisarawe, Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Margaret Mhando alisema watoto wakipewa nafasi ya kujifunza wanaweza kuwa mabalozi wazuri wa mambo ya kijamii.

Aidha Mhando alisema kwa kuwa ugonjwa wa malaria ndio unaoathiri zaidi watoto wa chini ya miaka mitano na kusababisha wastani wa vifo 60,000 kila mwaka nchini kuna haja ya kuwashirikisha watoto hasa kwa kuwaruhusu kusikiliza vipindi vinavyowaelimisha kujikinga na ugonjwa huo.

“Watoto wana ushawishi mkubwa kwa wazazi, wakielimishwa wanaweza kufikisha ujumbe kwa wenzao na jamii kwa ujumla. Vita ya Malaria ni ya washirika wote hivyo tushirikiane ili kuyatokomeza,” alisema Mhando.

Kwa upande wake Mkuu wa Mradi wa COMMIT unaoendeshwa na Kituo cha program za mawasiliano cha Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Robert Ainslie kwa kushirikiana na Wizara ya Afya-Mpango wa Taifa wa kudhibiti ugonjwa wa Malaria (NMCP) alisema wasikiliza mada mbalimbali kupitia radio za umeme wa jua zitakasosambazwa kwenye maeneo yao.

“Ili kuhakikisha kuwa watoto wengi hasa wanaoishi vijijini wanasikiliza kipindi cha PATAPATA, Mradi wa Commit utasambaza radio 2,000 kwa mawakala wa kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii (CCA) walioko kwenye kata ambao watawakusanyika na watoto kusikiliza na baadae kufanya majadiliano,” alisema Ainslie.

Vilevile Mkuu huyo wa Mradi wa COMMIT alisema lengo la mradi huo ni kuleta mabadiliko ya tabia na mienendo ya watu kuhusiana na matumizi ya vyandarua vilivyotiwa dawa, kujikinga na ugonjwa wa Malaria wakati wa ujauzito, kupata tiba sahihi ya ugonjwa huo na upuliziaji dawa kwenye kuta na paa za nyumba kwenye wilaya zenye maambukizi makubwa ya Malaria.


Asasi ya Keyoden ndio inayotekeleza mradi huu katika wilaya ya Kisarawe na moja ya shughuli zake ni kuandaa mabalozi wa Malaria kama wa shule ya Chanzige B. Commit ni mradi unaofadhiliwa na Mapango wa Rais wa Marekani wa kupambana na ugonjwa wa Malaria (PMI) kwa kupitia kitengo cha misaada cha watu wa Marekani USAID.
Habari kwa Hisani ya Jiachie Blog

No comments: