Hili ni Daraja la Kawe karibu na kituo cha jeshi cha mlalakuwa
Pembezoni mwa mto ambapo mataka taka yamekwama na kuhatarisha afya za watu
Maji haya yanatokea upande wa pembezoni mwa ukuta wa Kituo cha jeshi cha Mlalakuwa
---------
Ni eneo ambalo viongozi na watu mbali mbali wanaishi, Eneo hili la darajani limetupwa na hakuna anaeangalia utunzaji wa mazingira katika eneo hili Muhimu. Tukiachana na uchafu uliokithiri katika eneo hili pia kuna tatizo masaa ya usiku ambapo kuna vibaka waliokithiri na wanatumia nyenzo hatari kama kurusha nyoka kwa magari na wakati mwingine mijusi vyura na Kaa. Kamera yetu ilijitahidi kuonana na wananchi waishio maeneo hayo ya Jirani walidai kuwa pamoja na kuwa wanajeshi eneo hilo mlangoni kabisa lakini hakuna msaada wowote wanaoupata na kuwa hakuna Doria yoyote ile,wananchi wa eneo hili waliomba kuwe na ushirikiano na jeshi la Polisi katika doria ili kusaidia mara tatizo linapo jitokeza.
No comments:
Post a Comment