Kwanza wadau tulikaribishwa na kibao hiki hapa ambapo kiingilio kilikuwa kama kinavyo someka hapo juu
Tulipo ingia ndani ya eneo hilo tulistaajabu kuona mazingira mazuri na yakuvutia tulitegemea mengi sana
Kwa ujumla wadau eneo la huku ufukweni mwa bahari kupo poa sana na upepo ni mwanana
Kashehe ilianzia hapa, pale mdau mmoja alipo omba kwenda msalani,na kwa bahati nzuri kulikuwa na kibao kikubwa kilicho onesha Toilets zipo eneo lipi.
Na huu ndio ulikuwa muonekano wa Toilets hizo kwa nje Mdau alisita kuingia lakini kwa kuwa alitingwa ilimbidi ajimuvuzishe. Samahani kwa picha ya chini wadau
Na hii ndio hali halisi ya vyoo ilivyo kua katika eneo hilo ambalo watu wengi huenda kula maisha, Vyoo vyote vilikua na hali kama hii na hiki ndicho kilikua ni kisafi kulipo vyote, Hakuna maji ya kunawa mikono, hakuna kitu chochote kinacho saidia swala zima la afya. Wadau walijalibu kuonana na uongozi wa eneo hilo lakini ilishindikana.
Swali ni je Kwa mtindo huu magonywa ya mlipuko yataisha lini?
No comments:
Post a Comment