Habari zilizo tufikia punde asubuhi hii zinasema kwamba mfanya biashara mkubwa wa Jijini Mbeya jina halikuweza kufahamika mala moja ameuawa vibaya na watu wasio julikana usiku wa kuamkia jana, kwa mujibu wa taarifa zaidi zimesema kuwa asubuhi ya leo wakati mama mmoja akielekea kazini amekutana na mwili huo wa Marehemu ukiwa umekatwa katwa vibaya Pembezoni mwa nyumba yake. Hata hivyo familia ya marehemu walikuwa hawana taarifa zozote mpaka walipo ambiwa na mama huyo, Mwili wa Marehemu umepelekwa Hospitali kwa uchunguzi zaidi....Taarifa zaidi zitawajia na Jeshi la polisi wameanza kufuatilia tukio hilo la kinyama na Kusikitisha..Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kama ukisema kuwa ni mfanyabiashara mkubwa basi jina lake lazima uwe nao kwa wafanyabiashara wakubwa wapo wachache. Habari hii ilihitaji taarifa zaidi badala ya kuiapload katika hali hiyo. Inaonyesha wewe haupo mbeya na ha ta aliyekupa habari hiyo naye amesikia tu mtaani kitu ambacho ni hatari kwa tasnia ya habari. Fanya utafiti wakutosha kabla ya kuandika
Post a Comment