Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, May 20, 2011

BREAKING NEWS: MWENYEKITI HALMASHAURI RUNGWE AUWAWA KWA RISASI

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja ambaye ni diwani wa kata ya Kiwira ameuawawa kwa risasi usiku huu majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari lake kuelekea nyumbani kwake.
Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa alimiminiwa risasi kadhaa wakati akishusha mguu wake kutoka kwenye gari ili kuingia nyumbani kwake eneo la Kiwira.
Maiti yake inapelekwa hivi sasa hospitali ya Makandana kwa kuhifadhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo kwa ujumla linaaacha maswali mengi kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe na mkoa  kwa ujumla.
Taarifa zaidi mtaletewa kadiri zitakapopatikana kutoka Rungwe

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Hayo sasa ndio hatutaki kabisa katika ulimwengu tulivu.

Hebu niulize: SASA NYINYI MAJAMBAZI WENYE KUTOA ROHO YAMTU NAMNA HII, MTAKULA NYAMA YAKE? AU MUMEFAIDI NINI SASA?