Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, April 18, 2011

Tafakuri Yangu Ya Leo: Wabunge Wetu Wanajua Sana Kupiga Makofi Kuliko Kujenga Hoja!


                                                  ………napenda kuunga mkono hoja…….
                    ………waheshimiwa wabunge mnaunga mkono hoja?..Ndiyooooooooo!..........
   Hizi ndio  kauli kuu mbili kwa wabunge wetu ya kwanza ni ya baadhi ya wabunge ambao wakisimama hawaachi kusema kauli hiyo ya kuunga mkono hoja huku ya pili ikitumika mara nyingi na spika kwenye kufikia maamuzi mbalimbali ambapo wabunge wetu mara nyingi ni watu wa ndiyo. Inasikitisha sana!
   Wabunge wetu wamekuwa wavivu wa kujenga hoja wamepwaya sana kiasi cha kwamba wamebaki kuwa watu wa ndiyo tu hata kwa mambo ambayo hayana maslahi kwa taifa au hao wananchi wa majimboni mwao, inasikitisha kuona kuwa kila mwaka bajeti ya nchi imekuwa ya uchungu kama sio jasho na damu kwa mtanzania masikini, bajeti hizi zimekuwa zimeshindwa kumkomboa mtanzania kutoka kwenye lindi la umasikini lakini cha ajabu ni kuwa bajeti hizi zilipitishwa bungeni na wabunge wetu na iwapo wewe msomaji wangu unadhani huu ni mzaha au naongopa basi subiri hilo bunge la bajeti la mwezi juni utaona halihalisi jinsi wabunge wetu walivyopwaya kwenye kujenga hoja watapitisha bajeti itakayozidi kutukamua.
    Huwa nashindwa kuelewa hivi kuna wabunge wanaenda bungeni kusema ndiyo tena kwa makelele makubwa? utadhani hizo kelee zao za ndiyo zinaboresha shule za kata majimboni kwao? Au zinawasaidia mamia ya masikini wa jimboni kwao kuweza kujikimu kimaisha?  Wabunge hawa ndiyo huonekana majimboni kila baada ya miaka mitano kisha hawachaguliwi bali wanatumia fedha kununua uongozi na kwa bahati mbaya ndiyo hivyo TAKUKURU haina la kufanya na hata ikithubutu mara kibao watuhumiwa wanashinda kesi na kuachiwa huru kisa TAKUKURU wanakosea kufungua mashtaka, ajabu sana!
   Na hata baadhi ya wabunge wa vyama Fulani wakijitutumua kusema umezuka mchezo wa kitoto wa kuwazomea , inasikitisha kuona kuwa CCM ndiyo walikuwa vinara wa kuwazomea wabunge wa CHADEMA na hata kuna wakati wabunge wa CHADEMA wamemlaumu waziwazi spika Anne Makinda kuwa anakibeba chama chake cha CCM na hata wabunge wa upinzani wakijitutumua kupinga maamuzi legelege kwa nguvu ya hoja kwa bahati mbaya wenzao wa CCM wapo wengi hivyo wanatumia hoja ya nguvu kuzima hoja za wapinzani.
   Hivi wabunge wetu wanajua kweli kwanini wapo bungeni? Wanafahamu tabu tulizonazo? Hivi hawa wabunge wanaounga mkono hoja wanafahamu kuwa kuna ndugu zetu wako mahabusu kwa mwaka wa tatu sasa bila kusomewa kesi? Hivi wanafahamu kuwa kuna ndugu zetu wanaporwa ardhi kwa hoja za uwekezaji? Wanafahamu kuwa madini yetu yanazidi kuisha na kubakisha mashimo ya kuzalisha mbu wa maralia huku wenyewe hatufaidiki kitu? Hivi hawa wabunge wanafahamu kuwa kuna ndugu wamefeli kwenye shulee za kata kwasababu tu serikali inafanya mzaha na elimu? Hivi hawa watu wanafahamu kuwa ajali za bararani zinazidi kutumaliza kwa uzembe wa vyombo husika? Hivi hawa watu wanafahamu jinsi gani vijana wetu walipigwa pale Mlimani na Dodoma kwa sababu ya kudai nyongeza ya fedha za kujikimu kitu cha haki kabisa? Inauma sana waache mzaha kabisa sisi masikini wan chi hii tunateseka tu bila sababu za msingi haiwezekani tukaendelea kuwa masikini huku wanaotusababishia umasikini huo ni wao tunawajua , HAKIKA HAWA HAWAVUMILIKI MAANDISHI YASHAANDIKWA UKUTANI UNABII NI LAZIMA UTIMIE TU.
    Hivi kwani hawa wabunge wasioweza hata kuchambua mambo kwa hoja kwanini wasijiuzulu tu? Wanafanya nini bungeni? Au kuitikia ndiyo? Wanakera sana yaani wanakubali kila kitu kwanini lakini? Mbona wenzetu kule Uingereza wanajadili mambo kwa hoja? Au hapo Kenya mbona bunge lao si mchezo kwa jinsi wanavyojadili mambo kwa hoja , sisi tuna nini? tumerogwa ? mbona sisi ni watu wa ndiyo huku tukiendelea kudidimia kwenye umasikini wa kutisha? Naam! Tatizo ni wabunge wetu kupenda kupiga makofi  hata kwenye mambo yasiyotusaidia wamekuwa watu wa ndiyo sana wanauwezo mdogo sana wa kujenga hoja na kuzisimamia, tufanyeje? Tafakari!

Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai,
Nova Kambota Mwanaharakati,
Nipigie; 0717-709618(Tanzania) au +255717-709618(Nje ya Tanzania)
Tanzania, East Africa,
Jumatatu 18 April, 2011.

No comments: