Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 1, 2011

Hii ni kali zaidi Shangazi anaetoa ‘vikombe’ aibuka Magu

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro akizungumza leo katika kikao cha wadau wa usafiri wa kwenda kwa Babu Loliondo.

 Katika kudhibiti usalama, hali mbaya ya huduma za afya, malazi, chakula, maji na huduma nyingine kwa mahitaji ya mwanadamu Serikali mkoani mwanza kupitia kamati yake ya ulinzi na usalama imetoa taarifa kwa vyombo vya habari jinsi ilivyo jipanga kuhakikisha watu wake wanaosafiri kuelekea kijiji cha Samunge wilaya ya Ngorongoro kupata tiba wanapata tiba bila usumbufu na hatimaye kurejea kwa usalama.                                                                                                                                           
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema kuwa katika kipindi cha tiba ya babu wa Loliondo ofisi yake imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ikiwa ni pamoja na watu kuachwa njiani bila msaada wowote, kutofikishwa kwa mchungaji kupata tiba kutokana na ubovu wa vyombo vya usafiri na baadhi ya watu kupoteza ndugu zao bila taarifa.   

Kwa hisani ya Dullonet Tanzania

Soma Zaidi>>

No comments: