Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, March 25, 2011

TRA WAPASHWA, WANAUHARIBU MKOA WA MBEYA

 Baadhi ya wajumbe waliohudhulia mkutano wa Uwekezaji wilayani Mbozi ambapo TRA walipashwa wazi kuwa wamekuwa wakichangia wafanyabiashara kuhama mkoa huo na kuuacha ukipoteza heshima yake kutokana na uwekezaji kukosekana. Inaelezwa na Meneja wa kanda wa kituo cha uwekezaji kuwa imefikia hatua ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko lukuki yanayohusiana na mienendo na tuhuma zinazoihusu TRA kuwakamua damu wawekezaji mkoani mbeya.
 Mmoja wa watoa mada juu ya taratibu za kituo cha uwekezaji nchini TIC ambaye pia ni afisa elimu kwa umma bwana John Mnali akiwasilisha mada yake
 Mfanyabiashara mkubwa wilayani Mbozi Unyiha Associate bwana Charles Chenza akitoa malalamiko juu ya namna vibali vya msamaha wa kodi visivyowasaidia wawekezaji wadogo na badala yake kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa nchini kutokana na mlolongo na urasimu wa kupatikana kibali hicho
 Sehemu ya mabango yanayozungumzia shughuli za TIC nchini Tanzania

 Kazi ilianzia hapa baada ya Meneja wa Kanda wa kituo cha Uwekezaji alipoamua kupasua jipu hadhani kuwa "TIC na TRA vyote ni vyombo vya serikali, lakini hapa naomba nieleze wazi kuwa TRA imekuwa ikiwaona wafanyabiashara wa mkoa wa mbeya kama wakwepa kodi na hawaaminiki!!!, nimekuwa nikipokea malalamiko kila siku meengi yakiihusu TRA kuwanyanyasa wafanyabisahara, na hali hii nimeiona ni tofauti na mikoa mingine kama ARUSHA, DAR na Mwanza,  sasa sijui TRA Mbeya wapo makini hata kuliko Pale ambako kamishna wa  kodi yupo (DAR ES SALAAM) hebu tuwatendee haki wawekezaji manake tukifanya hivi tunadumaza uwekezaji mkoani mbeya.

Bw. DAUDI RIGANDA meneja TIC Kanda ya nyanda za juu kusini

No comments: