Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 22, 2011

IDADI YA VIFO AJALI YA BENDI YA FIVE STAR YAONGEZEKA , MAJINA 13 YATAJWA..


Majina ya wanataarabu wa bendi ya Five Star waliokufa katika ajali mbaya ya gari Mikumi mkoani Morogoro yamefahamika akiwemo Issa Kijoti, kiongozi wa bendi hiyo Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

Kwa mujibu wa taarifa hii ya uhakika uliyothibitishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro (RTO) zinadai kuwa waliokufa ni 13 majeruhi 8 na kuwa baadhi ya waliokufa wapo waimbaji ,wapiga vyombo ,mcheza show na mafundi mitambo japo majina ya majeruhi yatakuja hivi punde.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi majeruhi mmoja amekufa akiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akipatiwa matibabu na kufanya idadi kufikia watu 13
Hivi sasa ndugu wa marehemu hao wapo katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro wakiendelea kutambua miili ya wanamuziki hao .
Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema Peponi

No comments: