Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, May 19, 2016

TANESCO MBEYA LAWAMANI

 
Mkazi  wa Mtaa wa Jacaranda jijini Mbeya Proterce Chrispine Mpora alipokuwa akitoa malalamiko yake dhidi yaTanesco kwa waandishi wa habari.


Mkazi  wa Mtaa wa Jacaranda jijini Mbeya Proterce Chrispine Mpora akionesha nyaraka zake alipokuwa akitoa malalamiko yake dhidi yaTanesco kwa waandishi wa habari.

Mkazi  wa Mtaa wa Jacaranda jijini Mbeya Proterce Chrispine Mpora  akitoa malalamiko yake dhidi yaTanesco kwa waandishi wa habari. 
LICHA ya Serikali hivi karibuni kuwaagiza Mameneja wa Shirika la umeme (TANESCO) kuhakikisha wanatafuta wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma ya Umeme, hali hiyo ni tofauti jijini Mbeya baada ya mteja wake kukatiwa nishati hiyo kwa deni la kubambikiziwa.
Hali hiyo ilibainishwa  na mkazi mmoja wa Mtaa wa Jacaranda jijini Mbeya Proterce Chrispine Mpora alipokuwa akitoa malalamiko yake dhidi yaTanesco kwa waandishi wa habari.
Mpora alisema shirika hilo limemletea usumbufu mkubwa kwa familia yake na kusababisha kupata hasara hivyo analidai shirika la ugavi wa umeme TANESCO mkoani Mbeya Zaidi ya shilingi milioni 50 kwa madai ya kumsababishia hasara baada ya kukosa huduma kwa muda mrefu.
Alisema Shirika limemkatia umeme kwenye  Nyumba iliyopo  block namba 9  ambayo aliinunua kutoka shirika la Bima mwaka 2004 baada ya kubinafsishwa na serikali ambapo hapo kabla ilitumiwa na shirika la taifa la famasia NAPCO likisimamiwa na Meneja wa kanda Hussein Mugwaya.
Alisema baada ya kuuziwa nyumba hiyo alikuta hakuna huduma ya umeme ambapo aliingia kwenye mkataba mpya na TANESCO na  alirejeshewa umeme na kisha kuukata mwaka mmoja baadaye kwa madai kuwa mtanguliwa wake anadaiwa shilingi milioni 3.9.



Mpora alisema jitihada  za kutaka kurejeshewa huduma hiyo zimeshindikana na kuahidi kuiburuza TANESCO mahakamani ili kupata haki yake kutokana na majibu anayoyapata kutoka Tanesco yakimtaka amtafute Meneja wa NAFCO ili alipe deni lake ndipo naye apewe huduma.
“Mimi siwezi kumtafuta huyo Meneja ili alipe deni wakati mimi sihusiki na baada ya kuomba huduma Tanesco walinikubalia na kuniingizia umeme sasa awali hawakuona hilo deni, nimewasiliana na Mwanasheria wangu, haki za binadamu na ngazi zingine Tanesco wakishindwa kurejesha umeme nitawaburuza mahakamani na kudai fidia ambayo ilikuwa Milioni 50 lakini inazidi kupanda” alilalamika Mpora.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya,    Francis Maze alipoulizwa kuhusiana na kuwepo kwa mgogoro huo kati ya Shirika na mteja alikiri kuufahamu na kuongeza kuwa amekuwa akikaa meza moja kwa ajili ya kumuelewesha mteja lakini hakuna muafaka unaofikiwa.


 Alisema Kuhusu suala la kumkatia umeme  mteja huyo kumetokana na  mlalamikaji kutumia ulaghai kuunganishwa kwenye mfumo huo ambapo shirika lilimchukulia hatua afisa aliyehusika kwa kumfukuza kazi.


Aliongeza kuwa Ili kumaliza tatizo hilo Meneja  amemtaka mlalamikaji kumtafuta mpangaji wa zamani ambaye ni Hussein Mugwaya ili aje afunge mkataba wake vinginevyo yeye ataendelea kudaiwa deni hilo na kutopata huduma yoyote ya umeme.

No comments: