Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza katika moja ya vikao vyake vya kujitambulisha kwenye taasisi za Umma zilizopo mkoani Mbeya. |
MKUU wa
Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS)
Mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanajipanga kuboresha miundombinu ya barabara ili
kuinua uchumi kuendana na jografia yake.
Agizo hilo alilitoa alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Tanroads Mkoa wa Mbeya katika ziara yake ya kujitambulisha kwenye taasisi za Serikali zilizochini yake ambapo alisema Mkoa wa Mbeya una fursa nzuri na jografia yake ni ya kimkakati kiuchumi.
Alisema Tanroads wanapojenga miundombinu ya barabara watambue fursa za kiuchumi zilizopo na zinazotarajia kwa kuweka viwango vyenye ubora unaoweza kuuletea maendeleo Mkoa wa Mbeya.
Makalla alisema Mkoa wa Mbeya unafursa ya uwepo wa mipaka na nchi jirani, Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe, Hifadhi za Taifa na Bandari za Itungi na Kiwira ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya kusafirishia mizigo na bidhaa mbali mbali hivyo ni vema miundombinu ya kuyafikia maeneo hayo ikaboreshwa.
Alisema barabara zikiwa imara na zinapitika kwa urahisi zitasaidia kusafirisha mizigo kupitia badari na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambao matarajio ya baadaye ni kutua kwa ndege kubwa za mizigo kuja kubeba bidhaa kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu kusini.
Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa ameagiza Watumishi wa Tanroads kujiepusha kuwa na urafiki na Makandarasi bali wawe na mahusiano ya kikazi kwani itasababisha kushindwa kuwasimamia kwenye miradi wanayoisimamia hali inayopelekea kazi nyingi kufanyika chini ya kiwango na kinyume na mikataba.
Pia aligiza kuhakikisha alama za barabarani zinawekwa kila mahali panapotakiwa ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima na kwamba atahakikisha Kamati za ulinzi na usala za Wilaya zinahusika moja kwa moja kwenye ulinzi wa miundombinu ya barabara ili kuepusha wanaohujumu.
Awali akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Meneja Tanroads Mkoa wa Mbeya,Mhandisi Paul Lyakurwa alisema Mbeya imekuwa Mkoa wa kwanza wa kujengea alama za barabarani kwa zege tofauti na utaratibu kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa alama za Chuma na bati.
Alisema mwaka jana mwezi Novemba pekee katika barabara mpya ya lami ya Mbeya hadi Lwanjiro alama 17 zenye thamani ya shilingi Milioni 4.5 ziliibiwa kabla ya barabara hiyo haijakabidhiwa na mkandarasi.
Alisema kutokana na wizi huo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akishirikiana na Tanroads kuendesha kampeni kupitia mikutano ya hadhara na watendaji wa Mitaa na vijiji kupewa elimu juu ya ulinzi wa miundombinu hali iliyopelekea wizi kupungua na hivyo kuanza kurudishia miundombinu mipya.

No comments:
Post a Comment