Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira asilia Mlima Rungwe, Innocent Lupembe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na miti aina ya Mipaina iliyovamia hifadhi hiyo na mikakati ya kuiondoa. |
HIFADHI ya Mlima Rungwe uliopo katika Wilaya ya
Rungwe mkoani Mbeya iko hatarini kupoteza uoto wake wa asili kutokana na
kuvamiwa kwa miti ya kisasa aina ya mipaina inayopoteza Bainoai za mlima huo.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa Wiki na
Mkurugenzi msaidizi wa Shirika la kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira Kanda ya
Mbeya(WCS), Sophy Machaga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka
Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI)waliotembelea
hifadhi yam lima huo.
Alisema mlima huo una bainoai pekee zinazowezesha viumbe hai
na uoto wa asili kuendelea kustahimili lakini uwepo wa mimea vamizi aina ya
mipaina hupoteza sifa kutokana na sifa zake za kuharibu mazingira na kukausha
vyanzo vya maji.
Machaga alisema a
uvamizi wa miti ya kigeni (Pinus patula) iliripotiwa na WCS kwa mara ya kwanza
mwaka 2004 ikiwa imevamia hekta 64lakini baada ya hapo imeendelea kuongezeka na
kufikia zaidi ya hekta 100 eneo lililovamiwa.
Kwa upande wake Mhifadhi Mazingira asilia Mlima
Rungwe(TFS), Innocent Lupembe alisema tayari kuna mpango wa usimamizi ambao utaanza
kutekelezwa mwaka huu 2016.
Alisema katika mpango hu0 kuna mpango mdogo wa
kuondoa miti vamizi aina ya misindano (Pines) ambayo ni tatizo kubwa katika
hifadhi ya Mlima Rungwe kwani inahatarisha ikolojia yake.
“Katika kutekeleza mpango mdogo wa kuondoa miti
vamizi, hatua kadhaa tayari zimefikiwa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha andiko
(proposal) makao makuu TFS. Katika mpango huo mdogo tunataraji kufuata hatua
kadhaa ikiwa ni pamoja na kupima ujazo wa miti na eneo lililovamiwa kisha kutoa
elimu kwa jamii inayozunguka hifadhi juu ya kusudio la kuiondoa miti hiyo. Hii
itahusisha pia viongozi mbalimbali katika ngazi za kata na wilaya. Shirika la
WCS litasaidia katika kufanikisha zoezi hili. Aidha uondoaji wa miti hii
unatarajiwa kufaidisha TFS na jamii inayozunguka hifadhi” alifafanua Mhifadhi
huyo.
Aliongeza kuwa changamoto kubwa katika jamii
inayoizunguka hifadhi hiyo ni shule zake kukosa madawati hivyo baada ya kuvunwa
miti hiyo walitarajia kutengeneza madawati lakini imegunduliwa kuwa mbao zake
ni laini hazifai kwa madawati.
No comments:
Post a Comment