Wanachama wa TAJATI wakishiriki katika ujenzi la daraja la Mto Lupa wakishirikiana na wakulima wa Chama cha Msingi cha Igangwe Amcos katika Kata ya Mtanila wilayani Chunya. |
Wakulima wakivuka katika daraja la Mto Lupa baada ya ujenzi wake kukamilika |
WanaTAJATI wakivuka katika daraja baada ya kushiriki ujenzi wake uliofanyika katika kijiji cha Igangwe Kata ya Mtanila Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya |
Muonekano wa daraja baada ya ujenzi wake kukamilika |
Daraja likiwa tayari kwa matumizi ya binadamu kwa ajili ya kuvushia Tumbaku baada ya mavuno |
ILI kukabliana na vifo vinavyotokana na wananchi
kusombwa na maji katika wilaya ya Chunya, ufumbuzi umepatikana baada ya
wakulima wa zao la tumbaku wa Kijiji cha
Igangwe Kata ya Mtanila kujitolea kujenga daraja kwa fedha zao na nguvu kazi
ili kuepuka madhara makubwa waliyokuwa yakikabiliana nayo kipindi cha masika.
Wakulima hao kutoka chama cha
Msingi cha Igangwe Amcos wamejenga daraja linalounganisha kijiji cha Igangwe na
Vitongoji vya Shauri Moyo na Mtukula ili kurahisisha usafiri kwa wanafunzi na
wakulima wa Tumbaku kuelekea kwenye mashamba yao.
Akizungumza na Waandishi wa
Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI)
waliotembelea kijijini hapo na kushiriki ujenzi huo, Mwenyekiti wa Kijiji cha
Igangwe Lwitiko Mwambegele alisema kabla ya kujengwa kwa daraja hilo wakulima
wengi wamepoteza maisha kutokana na kusombwa na maji wakiwemo wanafunzi.
Mwambegele alisema wakulima
wengi hutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki kwenda mashambani hivyo mara
nyingi walikuwa wakipata ajali mara wavukapo mto Lupa na kupelekea kupoteza
maisha jambo waliloona ni vema kuchangishana na kujenga daraja imara.
“Wakulima wengi wamepoteza
maisha kwa kuangukua mtoni na kusombwa na maji na watoto wete wadogo ambao ni
wanafunzi lakini tukaona hatuwezi kuisubiri serikali ije itujengee na tukaamua
tuchangishane shilingi 20,000 kila mkulima ili kufanikisha zoezi hili ambalo
hadi sasa tumekamilisha kwa asilimia 95.
Alisema jumla ya shilingi
Milioni 2.5 zilipatikana ambazo zimesaidia kuchana mbao na kusomba kupeleka
eneo la mradi pamoja na ununuaji wa misumari na nguvu za wananchi zimetumika
kwa asilimia kubwa zaidi na vitendea kazi ambapo jumla ya mbao 313 zilichanwa
na kutumika.
Kwa upande wao baadhi ya
wakulima walioshiriki ujenzi huo walisema zoezi hilo limetumia muda wa mwezi
mmoja kutokana na michango kusua sua lakini kazi iliyofanyika imeokoa fedha
nyingi tofauti na serikali kama ingemuweka mkandarasi.
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI,
Christopher Nyenyembe aliwapongeza wananchi hao kwa kujitolea katika kazi za
maendeleo na kwamba ni mfano wa kuigwa badala ya kuitegemea serikali kwa kila
jambo hata kama wao wanauwezo nalo.
Alisema ni vema wakulima hao
wakaendelea kuainisha maeneo mengine kwa kuyafanyia kazi ambapo Serikali itaona
aibu na kuamua kuchangia na kusaidia nguvu za wananchi pindi wanapokwama
kukamilisha miradi waliyoinza.
“Kwa kutazama ujenzi wa daraja
hili lenye urefu zaidi ya mita 100 kama lingekuwa mikononi mwa mkandarasi
nadhani zaidi ya Sh milioni 200 zingetumika,wananchi wamefanya kazi kubwa sana
nay a ajabu” alisema Nyenyembe.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,
Sophia Kumbuli, alionyesha kushangazwa na kitendo cha Wananchi hao kujenga
daraja hilo na kuongeza kuwa wameisadia Serikali kwa kiwango kikubwa na kuokoa
fedha nyingi ambazo makadirio ya wataalam mradi huo ungekuwa wa mamilioni ya
fedha.
“Nawahakikishia lazima niende
nikajionee daraja hilo mimi mwenyewe ikiwa ni pamoja na kuwaongezea nguvu kwani
daraja naliona ni kubwa na kugharimu milioni mbili tu, hizo ni fedha ndogo kuna
kadaraja mkandarasi amekajenda hapo jirani kamegharimu zaidi ya milioni 60
hivyo wameokoa mamilioni ya shilingi nawapongeza sana” alisema Mkurugenzi huyo.
No comments:
Post a Comment