KATIBU mkuu wa Wizara ya Afya
na ustawi wa jamii ambaye awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya
Kanda ya Nyanda za juu kusini, Dk. Mpoki Ulisubisya amesema ushirikiano
unatakiwa ili kutekeleza mambo mbali mbali aliyoyaacha.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya, Dk. Ulisubisya alisema
hakutarajia kama Rais Dk. Magufuli angeweza kumpa majukumu na kumteua katika
nafasi kubwa jambo lililomshtua kwa kiasi kikubwa.
Alisema kichwani kwake alikuwa anajipanga
kuhakikisha anatekeleza majukumu aliyokuwa ameachiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu
Wizara ya afya na ustawi wa jamii wiki mbili zilizopita Donan Mbando aliyefanya
ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda.
Alisema katika ziara hiyo Mbando
aliagiza kuhakikisha umaliaziaji wa jingo la maabara ya kupima virusi vya Ebola
unakamilika haraka ndani ya wiki mbili na kuanza kutoa huduma, ujenzi wa jengo
la vipimo mbali mbali kama Utra saund,
CT Scan na X – Ray.
Alisema agizo lingine lilikuwa
kuhakikisha Hospitali hiyo inaanzisha Chuo kikuu kwa ajili ya kuongezea taaluma
kwa madaktari na kuboresha huduma za dharura na kupunguza foleni kwa wagonjwa
mambo ambayo tayari alianza kuyafanyia kazi na kuyawekea mikakati.
Aidha alitoa wito kwa waandishi
wa habari kuendelea kuandika habari za kuisaidia hospitali na madaktari ili
waweze kurekebisha kasoro zinazokuwepo lengo likiwa ni kuhakikisha Hospitali
hiyo inakuwa mfano kitaifa kwa utoaji wa huduma bora.
Dk. Ulisubisya pia alitoa wito kwa waandishi wa habari
kuendelea kumpa ushirikiano Mkurugenzi mwingine atakayechukua nafasi yake ili
kuhakikisha mipango yote inakamilika kama ilivyokuwa imepangwa.
No comments:
Post a Comment