Katibu wa Alumni, Graciano Kunzugala, akiwashukuru washiriki wa Mafunzo ya Ujasiliamali waliyoyapata wahitimu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya |
Profesa Mjema akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya ujasiliamali kwa wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya. |
Baadhi ya washiriki wa semina ya ujasiliamali wakisubiri kutunukiwa vyeti vya ushiriki wa mafunzo waliyopata |
Mkurugenzi wa CBE Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akimwelekeza jambo Mwenyekiti na Katibu wa ALUMNI Kanda ya Mbeya |
Profesa Mjema akimtunuku Cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali mmoja wa Wahitimu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya. |
Mhitimu wa CBE akipongezwa na Mkurugenzi wa Kampasi ya Dodoma |
Mkurugenzi wa Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akimpongeza mmoja wa wahitimu wa CBE Mbeya baada ya kutunukiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali |
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi na baadhi ya Watumishi wa CBE baada ya kufungwa kwa mafunzo ya ujasiliamali |
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali wakionesha vyeti vyao katika picha ya pamoja na viongozi wa CBE na waandaaji wa mafunzo |
MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE), Profesa Emmanuel Mjema,ametoa wito kwa wahitimu wa vyuo kutokata tama katika
utafutaji wa maisha.
Profesa Mjema ametoa wito huo alipokuwa
akifunga mafunzo ya siku mbili ya Ujasiliamali kwa Wahitimu wa CBE Kampasi ya
Mbeya yaliyomalizika katika ukumbi wa Hoteli ya Livingstone.
Profesa Mjema ambaye pia aliwatunuku
vyeti vya kuhudhuria mafunzo hayo wahitimu alisema katika utafutaji wanapaswa
kuwa na uvumilivu hivyo hawatakiwi kukata tama mapema.
Aidha aliwataka wahitimu hao kuitumia
kwa vitendo elimu ya ujasiliamali walioipata kufanya kazi kwa bidii ili kuleta
maendeleo katika jamii.
Mkuu huyo wa Chuo pia aliwapongeza
waandaaji wa mafunzo hayo ambao ni umoja wa wahitimu waliosoma zamani
CBE(ALUMNI) kanda ya Nyanda za juu kusini.
Alisema kitendo walichokifanya ni
uzalendo wa kukipenda Chuo kwa kurudisha fadhila ambayo wameitoa kwa wahitimu.
Alisema jukumu la wahitimu ni
kukishauri Chuo juu ya mabadiliko mbali mbali na kukijulisha juu ya mambo
yanayokuwa yakiendelea nje ya Chuo.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti
wa ALUMNI Kanda ya Nyanda za juu kusini, Boyd Mwakyusa alisema mafunzo hayo
yamehudhuriwa na washiriki 88.
Alisema lengo la mafunzo ni kuwafanya
wahitimu kutohangaika pindi wanaporudi uraiani badala yake wajue fursa za
kuzitumia ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na ujasiliamali.
No comments:
Post a Comment