Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, Dk. Donald Mbando akitembelea miradi katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, Dk. Donald Mbando akipata maelezo juu ya ukamilishwaji wa jengo la vipimo vya uchunguzi katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, Dk. Donald Mbando akitoa maelezo kuhusu mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya Tehama. |
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya
na ustawi wa jamii, Dk. Donald Mbando, ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda iliyopo mkoani Mbeya kuhakikisha inakamilisha
ukarabati wa maabara ya kupimia magonjwa yanayoambukiza haraka ikiwemo Ebora.
Dk. Mbando alitoa maagizo hayo
jana alipofanya ziara katika Hospitali hiyo kwa lengo la kufuatilia miradi ya
idara ya afya inayotekelezwa ikiwemo Hatua za ukarabati wa maabara, ukarabati
wa Wodi za wagonjwa na ujenzi wa jingo la vipimo vya uchunguzi.
Akizungumza na uongozi wa
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Katibu mkuu alisema lengo la ziara yake ni
kukagua na kuangalia miradi ya maendeleo ili kujua hatua ilipofikia katika
kipindi ambacho serikali inaenda kuandaa bajeti.
Alisema lengo la kutoa wiki mbili
kukamilisha ukarabati wa jingo la maabara ili liweze kuanza kutumika kutokana
na uwepo wa tishio la ugonjwa wa mafua makali kuikumba dunia hivyo kuokoa
gharama za kusafirisha sampuli za wagonjwa kwenda nje ya nchi.
Pia Katibu Mkuu aliagiza
uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha ndani ya wiki moja analetewa mchanganuo
wa fedha za kumalizia ujenzi wa jingo la vipimo vya uchunguzi ili kuweza
kuombea fedha kutoka serikalini kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambapo Milioni
500 zilishatolewa katika ujenzi wa awamu
ya kwanza.
Alisema jingo hilo likikamilika
litasaidia kurahisha upatikanaji wa vipimo kwa wagonjwa kirahisi na
kuwapunguzia gharama za kusafiri wananchi kwa ajili ya kufuata vipimo jijini
Dar es salaam ili hali uwezekano wa kupata Mbeya upo kutokana nawataalam
kuwepo.
Alisema kukamilika kwa jengo hilo
kutarahisisha kupatikana kwa vipimo aina ya X- ray, ultra sound, ct scan na
mashine zingine kwa ajili ya wagonjwa kutoka mikoa saba inayotegemea huduma
katika Hospitali ya Kanda ya Mbeya.
Katibu mkuu pia aliagiza
Hospitali zote nchini kuanzia Hospitali za Wilaya, Hospitali za Mikoa na Hospitali
za Rufaa za Mikoa na Kanda kuhakikisha
zinakuwa na mfumo wa Elekitroniki kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato ili
kupunguza mwanya wa upotevu wa fedha na ubadhilifu.
Alisema mfumo huo pia utasaidia
kurahisisha mawasiliano baina ya madaktari kwa madaktari au Hospitali moja na
nyingine kuhusiana na tatizo la ugonjwa pindi tatizo linapokuwa mkubwa na
msaada unahitajika.
Aidha aliupongeza uongozi wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato baada ya
kuanzisha mfumo wa TEHAMA ambapo kabla ya mfumo huo walikuwa wakikusanya
Milioni 50 kwa mwezi lakini sasa zinakusanywa shilingi Milioni 500.
Katika agizo la nne, Katibu
Mkuu ameitaka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kubuni huduma za miradi ili
kuongeza mapato zaidi kama vile kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti ili kutoa
huduma ya haraka nakiwango cha juu, utengenezaji wa maji ya dawa(IV – Fluids)
na vilainishi vya mafuta ya ngozi pamoja na uanzishwaji wa Chuo kikuu kwa ajili
ya kuinua elimu za watumishi wa Idara ya afya.
No comments:
Post a Comment