Baadhi ya wazazi na wageni mbali mbali wakiwa kwenye sherehe za Mahafali.
MKUU wa Wilaya ya Mbeya,
Nyerembe Munasa amewataka wamiliki wa Shule binafsi kuwa na maono ya kupanua
wigo wa utoaji wa elimu ili kuleta ushindani wenye tija kwa Taifa.
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa rai
hiyo hivi karibuni katika sherehe za Mahafali ya Pili ya Chekechea (top class)
ya Shule ya Msingi na awali ya Gamaliel iliyopo Lyoto jijini Mbeya.
Nyerembe alisema elimu ni jambo
muhimu katika maendeleo ya taifa lolote duniani hivyo ni wakati muafaka kwa
wamiliki wa shule binafsi kuwekeza katika kutoa elimu yenye ushindani bila
kuogopa.
“ Napenda nitoe wito sasa kwa
wamiliki wa shule hii baada ya kuwa na madarasa ya awali na Msingi fikirieni
kuanzisha shule ya Sekondari na baadaye Chuo ili watoto wanaotoka hapa waweze kuwa
na mwendelezo mzuri kutokana na misingi waliyokulia” alisema Mkuu huyo wa
Wilaya.
Aliongeza kuwa ili waweze
kufanikisha hayo ni vema uongozi ukawa na malengo makubwa hususani kuweka uwekezaji katika ufundishaji
wa masomo ya sayansi ili kufikia matarajio ya Serikali kuwa na wataalamu wengi
wa sayansi.
Alisema pia uongozi wa Shule
hiyo unapaswa kuzingatia lishe kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo
kutokana na kuwa na umri mdogo ili waweze kukua wakiwa na afya imara
itakayowasaidia kushika vizuri masomo yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule
hiyo, Edward Olesaka alisema Wazazi
wasiwe na shaka juu ya uwepo wa watoto wao shuleni hapo kwani elimu wanayoipata
ni bora kwa kuwa walimu wanazingatia majukumu yao kikamilifu.
Naye mmoja wa Wakurugenzi wa
Shule hiyo, Subilaga Mwambeta alisema ushauri uliotolewa na Mkuu wa Wilaya
utaanza kufanyiwa kazi ambapo hivi sasa shule hizo zimeshaanza kupata usajili
kutoka Serikalini.
Alisema ushirikiano ambao
Serikali inaonesha katika shule binafsi unazidi kuwapa nguvu ya kupanua wigo wa
utoaji wa elimu kwa watanzania.
|
No comments:
Post a Comment