Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 25, 2015

TAASISI YA UTAFITI YA VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI (ESAURP)YAANDAA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO MKOANI MBEYA


Mmoja wa wakufunzi wa masomo ya ujasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Dar es salaam Profesa Humphrey Mushi akizungumza katika semina ya ujasiriamali inayotolewa na Taasisi ya utafiti ya vyuo vikuu vya afrika na kusini mwa Afrika ( ESAURP) kwa wafanyabiashara ndogondogo mkoa wa mbeya katika ukumbi wa shule ya St.Agrey jijini Mbeya Agosti 24 mwaka huu.
Mwakilishi wa Taasisi ya Esaurp kutoka jijini Dar es salaam Ndugu Peter Celestine akizungumza katika mafunzo hayo ya siku tano yaliyolenga kuwapatia wajasiriamli hao Ujuzi ,Mbinu ,maarifa pamoja na stadi za biashara ili kuwezesha ukuaji wa biashara zao.
Baadhi ya wajasirimali kutoka maeneo tofauti tofauti Mkoani mbeya wakiendelea kupatiwa mafunzo.
Mmoja wa walimu katika mafunzo hayo Ndugu Upendo Mwinuka akizungumza na wajasirimali hao hawapo Pichani.

Afisa Mikopo kutoka Benki ya Posta Tanzania Mbeya( TPB) Ndugu Tresphory  Mtwele akizungumza na wajasirimali hao ili kuwashawishi kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo ya riba nafuu na benki hiyo.

 Picha Emanuel Madafa Mbeya(JAMIIMOJABLOG)

2 comments:

Anonymous said...

Tunaomba muache kutumia jina la Mbeya Yetu kwani habari zinaztoka ni za upande mmoja wa CCM. Je hi ni blog ya CCM? Hamna maadaili ya uandishi wa habari. AIBU tena AIBU!

Anonymous said...

Habari zenu za upendeleo upande mmoja, achene hizo!