.Waandishi wa habari wakichukua maelezo kutoka kwa wahanga wa
tukio la kukatwa kiganja kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino).
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi
Stella Manyanya walifika Hospitalini baada ya mtoto huyo kufikishwa
kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mtoto
huyo mkazi katika kijiji cha Ikonda kata ya Chitepa wilaya ya Sumbawanga mkoani
Rukwa alihamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kukatwa kiganja
chake akitokea kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani hapa.
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo, Prisca Shaban(28) alisema tukio hilo
lilitokea juzi majira ya saa saba usiku alipokuwa anarudi ndani akitokea nje
kujisaidia alivamiwa na mtu ambaye hakumfahamu na kisha akamsukumia ndani kabla
ya kumpiga kichwani kwa rungu na kisha kupoteza fahamu.
Alisema
akiwa amepoteza fahamu mtu aliyekuwa amemvamia ndipo alipata nafasi ya kuingia
ndani na kutekeleza adhma yake ya kumkata kiganja mtoto huyo ambaye ni mmoja
kati ya watoto watatu wenye ualbino katika familia hiyo na kuondoka
nacho.
Alisema
wakati hayo yakitokea mumewe aliyemtaja kwa jina la Cosmas Lusambo alikuwa
amekwenda kulala nyumbani kwa mke mdogo kwani ilikuwa zamu ya kwenda kulala
huko kwa usiku huo lakini baada ya kusikia mayowe ya kuomba msaada alikwenda
kuungana na familia yake na kumpeleka mtoto kituo cha afya cha Kamsamba
kutokana na kuwa jirani na kijiji chao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Akizungumza baada
ya kumtembelea Baraka katika wodi ya watoto kwenye hospitali ya rufaa kanda ya
Mbeya, alioneshwa kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili
wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua.
Alisema
ni tukio ambalo linasikitisha ambalo linazidi kuendeleza vitendo vya aibu kwa
kuwafanyia ukatili wa kinyama albino kwa ujinga wa watu wachache
wanaowadanganya watu kuwa viungo vyao ni bahati ya kuleta utajiri.
Mhandisi
Manyanya mbali na kuzungumza na familia ya waathirika wa janga hilo pia aliongoza
sara fupi ya kuwaombea albino hospitalini hapo alionesha pia kusikitishwa na
mwenendo wa mashitaka ya watu waliofanya ukatili dhidi ya albino akisema
mahakama zimekuwa na milolongo mirefu inayokatisha tama wadau wa kupinga
ukatili huo.
Mkuu
huyo wa mkoa alishauri pia kuangaliwa upya kwa sheria inayohusu masuala ya
hukumu za kifo akisema ikibidi inapaswa kubadilishwa ili iweze kutoa haki kwa
watu wanaofanya ukatili dhidi ya wenzao.
Alisema
sheria ya sasa kumtaka rais pekee kuwa mtu wa mwisho kutoa uamuzi kunyongwa kwa
mtu aliyehukumiwa inakosa nguvu ya kutekelezwa kutokana na majukumu mengi
aliyonayo na kushauri kuwa ni vyema vyombo vya sheria vipewe mamlaka ya mwisho
ya kutekeleza adhabu hiyo.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment