Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 19, 2015

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA NA KUMI NA NNE KUKIMBIZWA HOSPITAL YA IGOGWE BAADA YA AJALI YA GALI KUBWA LA MAFUTA YA PETROL T821ARF KUANGUKA KIJIJI CHA ISONGOLE (NO ONE) WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA IKIWA NI ENEO HILOHILO MITA CHACHE ILIPOTOKEA AJALI ILIYOUA WATU WENGI KWA TUKIO KAMA HILI NA KUZIKWA KATIKA KABURI MOJA

SEHEMU ILIPOTOKEA AJALI YA GALI T821ARF KATIKA KIJIJI CHA ISONGOLE (NO ONE) NA KUSABABISHA WATU WATATU KUFA NA KUMI NA NNE WAKIWA WAJERUHI NA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPITAL YA IGOGWE WILAYANI RUNGWE HUKU WATU WATATU WAKIWA KATIKA HALI SIO NZURI

CHANZO CHA MOTO KIKIWA NI MAFUTA YALIYOKUWA KATIKA MTALO HUU AMBAPO MAMA MMOJA AKAENDA NA KIBATALI KUANGALIA YANAYOPITA MTALONI NI MAFUTA AU MAJI NDIPO MAFUTA YAKASHIKA MOTO WA KIBATALI  NA KUSABABISHA MOTO MKUBWA KWENYE TUKIO


MABAKI YA GALI SCANIA T831ARF BAADA YA KUPATA AJALI NA KUWAKA MOTO AMBAPO WAKAZI WA ISONGOLE WANASEMA KUWA MOTO ULIKUWA MKUBWA SANA NA KUZIMA INGEKUWA NGUMU HIVYO KIKOSI CHA ZIMA MOTO KUTOKA JIJI LA MBEYA WALIFIKA  USIKU HUO KWA WAKATI MWAFAKA KUFANIKIWA KUZIMA MOTO KWAKUWA MAAFA YANGEKUWA MAKUBWA BAADA YA BAADHI YA NYUMBA ZILIANZA KUSHIKA MOTO
ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKAFIFA KATIKA KIJIJI CHA ISONGOLE NA KUWAPA POLE WAFIWA NA MAJERUHI KATIKA HOSP YA IGOGWE HUKU AKIWATAKA WANANCHI KUACHA TABIA MBAYA YA KUKIMBILIA AJALI ZITOKEAPO NA KUPORA VITU MBALIMBALI PIA KUKIMBILIA MAGALI YA MAFUTA AMBAYO MOTO UTOKEAPO MAAFA YANAKAUWA MAGUBWA KAMA YALE YALIYOTOKEA MIAKA YA NYUMBA NA WATU WENGI KUZIKWA KATIKA KABURI MOJA HUPU LEO TUKIO LIKIWA KAMA LILILOPITA WANANCHI KUKIMBILIA KUCHOTA MAFUTA,  HUKU MAMA MMOJA AKIENDA NA KIBATALI KUANGALIA MTALON JE NI MAFUTA AU MAJI YANAYOPITA KARIBU NA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA KULIPUKA KWA MOTO MKUBWA AMBAO UMEUA WATU WATATU HADI SASA NA WATU KUMI NA NNE WAKIENDELEA NA MATIBABU

WANANCHI WAKIMSIKILIZA MKUU WA POLISI TUKUYU MWENYE KOTI JEUSI KULIA AMBAYE NAYE AMEWATAKA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUKIMBILIA MATUKIO YA AJALI


DIWANI WA KATA YA ISONGOLE AKIONGEA NA WANANCHI WAKE HUKU AKIWATAHADHARISHA SANA KUACHA TABIA MBAYA YA KUKIMBILIA AJALI NA KUIBA VITU AU KUCHUKUA MAFUTA AMBAYO MOTO UNAPOTOKEA BASI MAAFA YANABAKI KWA WAKAZI WA ISONGOLE

MMOJA WA WAGOJWA  WALIO KATIKA HALI MBAYA KATIKA HOSPITAL YA IGOGWE WAKIENDELEA NA MATIBABU


MMOJA WA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO AKIUGULIA VIDONDA NA MAUMIVU YA MOTO

KUSHOTO DEREVA WA GARI LILILOPATA AJALI ZAWADI NYATO AKIWA NA MKEWAKE NA KAKA YAKE KATIKA HOSPITAL YA IGOGWE TUKUYU AKIWASIMULIA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA KUWA "NILIPOKUWA NASHUKA MITELEMKO YA ISONGOLE KARIBU NA KABURI PALE JUU NIKAONA TAA ZA UPEPO WA KALI LANGU HAZIWAKI NA NIKAONA GALI HALIKAMATI BREKI HIVYO KWAKUWA NILIKUWA NA MZIGO MZITO GALI LIKANISHINDA NA SASA NAJIKUTA NIPO HOSPITALI ILA HADI HAPA SIJAELEWA KILICHOYTOKEA

DR WA ZAM FRADY YUSUFU AKIWA ANAONGEA NA KINGOTANZANIA AMESEMA KUWA USIKU WAMEPOKEA MAJERUHI WA MOTO WAPATAO KUMI NA KUMBI NA NNE HUKU WATATU HADI SASA HARI ZAO SIO NZURI SANA LAKIN WENGINE WANAENDELEA VIZURI NA MATIBABU

MUONEKANO WA KIJIJI CHA ISONGOLE AMBAPO HUTOKEA AJALI NYINGI ZINAZOHUSISHA MAGALI KUANGUKA NA WAKAZI WA HAPA WAKIWA NA HISTORIA YA KUKIMBILIA AJALI MBALIMBALI NA KUPOLA VITU HUKU IKIWA KAWAIDA KWA WAKAZI HAO KUKIMBILIA KUCHOOTA MAFUTA AMBAYO HUWAPEREKEA KATIKA JANGA KUBWA LA MOTO

HILI NDILO KABURI LA WATU WALIOUNGUA NA MOTO MIAKA KADHAA ILIYOPITA IKIWA NI KUMBUKUMBU ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA  ISONGOLE ( NO ONE) AMBAPO HADI SASA HAIELEWEKI NI WATU WANGAPI WALIZIKWA KATIKA KABURI HILI ILA KWA WENYEJI WANASEMA KUWA NIZAIDI WATU 45  WAKIKUFA KATIKA AJALI HIYO



Watu watatu wamefariki dunia kwa ajari ya moto akiwemo utingo wa gari hilo aliyefia hospitari kwa kuvuja damu nyingi na watu kumi na nne kujeruhiwa na kulazwa katika hospitari ya Igogwe na watutu kuthibitishwa na Dactari kuwa hali zao ni mbaya baaada ya gari aina ya scania lenye namba za usajiri T821ARF mali ya kampuni ya Irasi likiwa limebeba mafuta ya petrol, kuacha njia  na kupinduka mida ya saa tatu usiku eneo la kijiji cha Isongole (namber one )kata ya Isionje .


Moto huo uliosababishwa na mwanamke aliekuwa na kibatari kwenda kumulika mafuta   katika mfereji wa maji uliopo eneo la tukio kwa kibatari chake  ili ajue kama yale ni mafuta au maji  kitendo kilichosababisa moto kuwaka kufuata mafuta yaliyo kuwa yakimwagika mpaka eneo gari lilipoanguka hivyo kusababisha watu mifugo na mashamba kushika moto.


Moja wa shuhuda wa tukio aliyejitambulisha kwa jina  moja la Matola amesema kwamba gari lilianguka mida ya saa tatu usiku ndipo wananchi walikimbilia kuchota  mafuta na dereva na baabhi ya wakazi  aliwaktaza  kusogea eneo hilo na kuwataka wawasaidie kutoka eneo hilo na baada ya mda kidogo wao kutolewa  ndipo moto ulilipuka kutoka katika mfereji  wa maji na kusambaa kufuata mafuta yalipo hadi kufika kwenye gari.


 Bwana Matola alifafanua kuwa“ Tunashukuru moto uliwahi kuwaka kabla ya watu kujaa hata hivyo baadhi  ya wenyeji wa eneo hilo walijitahidi kuzuia watu wasichote mafuta lakini wengine hawakuweza kuwasikiliza wakizani kwamba watapata mafuta kama ilivokuwa juzi (siku tatu nyuma )baadaya gari la mafuta ya dizeli kuanguka na wao kuchota mafuta mengi na kuuza lita ishirini kwa shilingi elfusaba tu, hadi alipotokea mama moja ambae ni moja wa waliofariki kuja na kibatari kumulika mferejini ili kujua kama yale ni mafuta au maji na ndipo mafuta yakashika moto.” 


Dereva wa gari hilo Zawadi nyato aliyekimbizwa hospitali ya igogwe baada ya kupata ajari amesema kuwa alipokuwa kwenye mlima anashuka taa ya upepo iliwaka kuashiria hakuna upepo na kwa sababu alikuwa amebeba mzigo mzito gari likamshinda na kujikuta yuko hospitalibila kujua kilichoendelea hapo.


Nae mkuu wa wilaya Mhe. Chrispin meela amefika eneo la tukio kutoa pole na lambi rambi kwa wakazi wa eneo hilo na kuwakumbusha kuwa  wawe makini na vitu vya hatari kama hivi kwani tukio kama hili liliwahi kutokea katika mtaa huo huo na kusababisah vifo vya watu wengi lakini bado wanarudia kitendo kama hicho. Hivyo amewataka watu wabadilike na wajifunze kupitia matukio yaliyopita.


Ajari ya moto kama hii iliwahi kutokea miaka ya 1990s katika kata hiyohiyo ya Isionje mtaa wa numba one mita chache  kutoka ilipotokea ajali hii ya leo na kuuwa watu wengi waliozikwa kwa pamoja katika eneo hilo kwani walishindwa kutambulika na ndugu zao na kijeruhi mamia ya watu.

  Kwa hisani ya 
TUMAIN OBEL

KINGO TANZANIA
Rungwe

1 comment:

Anonymous said...

Elimikeni wandugu, huwezi kupata utajiri wa siku moja tu. Unakimbilia kifo baada ya kuepuka kifo nani alaumiwe? Mutaanza kumsingizia Mungu hali Mungu si chanzo cha kifo chako. Anyway, wapumzike kwa amani waliokufa na majeruhi wapate unafuu na kurudi katika shughuli zao za kila siku.