Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Vanessa,
Shukran Gidion akisalimiana na Msanii wa Filamu Charles Magari.
|
Mkurugenzi wa Vanessa Sekondari wakijadiliana
jambo na msanii Mzee Magari.
|
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Vanessa, Exon
Mwakalikamo, akisalimiana na Mzee Magari.
|
Msanii mkongwe wa Filamu nchini, Charles Magari akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Shule ya Vanessa Sekondari. |
.Mzee Magari na baadhi ya wasanii, waandaaji wa
filamu na watengenezaji wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari Mbeya.
|
Magari akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari. |
Mzee Magari akiwa na Mkurugenzi wa Vanessa pamoja na baadhi ya wasanii wakijadiliana jambo |
Mwandaaji wa Filamu ya Black Valentine
inayotaraijiwa kuzinduliwa, Yekonia Watson akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari.
|
Mkuu wa Shule ya Vanessa Exon Mwakalikamo
akielezea lengo la shule hiyo kushiriki katika filamu ya Black Valentine.
|
Baadhi ya Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakiendelea
na majukumu yao ya kuchukua habari.
|
WASANII wakubwa wa Filamu nchini wametakiwa
kuacha kuwatoza gharama kubwa wasanii wachanga pindi wanapokuwa wameombwa
kushiriki katika moja za kazi zao.
Rai hiyo imetolewa na msanii nguli wa Filamu
nchini, Charles Magari maarufu kwa jina la Mzee Magari alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano wake uliofanyika kwenye ofisi za shule ya
Sekondari ya Vanessa iliyopo Isyesye jijini Mbeya.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kutoa taarifa
kwa jamii kuhusiana na uzinduzi wa Filamu iitwayo Black Valentine inayotarajia
kuzinduliwa kesho katika kilele cha siku ya wapendanao(Valentine day) uzinduzi
utakaofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda sunset Soweto jijini Mbeya.
Magari alisema mara nyingi wasanii wa Dar es
salaam wamekuwa wakilalamikiwa na wasanii wa mikoani kuhusu kutoa majibu ya
kukatisha tama pale wanapopigiwa simu wakiombwa kushiriki kwenye kazi zao
sambamba na gharama kubwa huku wakisahau kama nao walianza chini.
Aliongeza kuwa pamoja na gharama kubwa
wanazowatajia wasanii wachanga bado hucheza nafasi ndogo kwenye hizo kazi jambo
ambalo huwakatisha tamaa watazamaji ambao wanakuwa na hamu ya kumuona msanii
mkubwa jinsi alivyoshiriki.
“ Mimi binafsi najivunia rekodi niliyonayo
ambayo naamini hakuna msanii ambaye ameweza kuifikia kwani nimeshiriki katika
Filamu kutoka Mikoa yote hapa nchini, gharama zangu ni nafuu kwani naelewana na
mwandaaji pia napenda kucheza kuanzia scene tano kwenda mbele ili mashabiki
wangu wafurahi uwepo wa mimi kwenye Filamu” alisema Mzee Magari.
Aidha Magari aliwataka wakazi wa Mbeya
kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo kwani licha ya yeye kualikwa kama
mgeni rasmi pia atatoa burudani kwa kutumbuiza nyimbo zake ambapo hadi sasa ana
albamu moja yenye nyimbo 6 yenye jina la Dar raha.
Kwa upande wake Mwandaaji wa Filamu ya Black
Valentine, Yekonia Watson maarufu kwa jina la Aman, alisema watu wajitokeze
kuangalia vipaji vya wasanii kutoka Mbeya walioshiriki katika Filamu hiyo
sambamba na kujionea utofauti wa Valentine iliyozoeleka na iliyochezwa kwenye
mkanda huo.
Aidha alitoa wito kwa Wakazi wa Mkoa wa Mbeya
kuacha kushabikia kazi za wasanii kutoka nje ya mikoa yao kwa kuchangia na
kuwaunga mkono wazawa kwa kununua kazi zao.
Alisema katika filamu hiyo iliyotengenezwa na
Enea Production imepata msukumo mkubwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule ya
Sekondari ya Vanessa, Shukran Gidion, ambaye ameanzisha utaratibu wa kufundisha
wanafunzi wake masomo ya sanaa pamoja na kushiriki katika filamu
hiyo.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment