PRF.
PETER MSOLWA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MAJI KILIMO NA UFUGAJI
AKIONGEA NA WANANCHI WA KATA YA MASOKO WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA
, MWENYEKITI NA KAMATI YAKE WALIPATA WAKATI MGUMU WA
KUPOKELEWA KATIKA MRADI WA MAJI WA MASOKO KUTOKANA NA JINSI MRADI
UNAVYOTEKELZWA KWA KUSUASUA
PRF.
PETER MSOLWA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MAJI KILIMO NA UFUGAJI
AKIONGEA NA WANANCHI WA KATA YA MASOKO WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA
,(HAWAPO PICHANI ) MWENYEKITI NA KAMATI YAKE WALIPATA WAKATI MGUMU WA
KUPOKELEWA KATIKA MRADI WA MAJI WA MASOKO KUTOKANA NA JINSI MRADI
UNAVYOTEKELZWA KWA KUSUASUA
WA
PILI KULIA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE EZEKIA MWAKOTA
AKIONGA NA WANANCHI KATIKA MOJA YA MIRADI ILIYOTEMBELEWA NA KAMATI
CHRISTINA
MSENGI MHANDISI WA MAJI WILAYA YA RUNGWE AKIELEZA JINSI CHANGAMOTO
MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI WAKATI WA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI WILAYANI
RUNGWE HUKU KELO IKIWA NI MRADI WA MAJI WA MASOKO MRADI AMBAO UMESIMAMA
HUKU WANANCHI WAKIHITAJI MAJI PASIPO NA MAFANIKIO TANGU MWAKA 2012 HADI
SASA MAJI HAKUNA
PICHA
YA PAMOJA KAMATI YA BUNGE MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NA WATENDAJI WA
HALMASHAURI YA RUNGWE KABLA YA KUTEMBELEA MIRADI YA MAJI
Wananchi wa
kata ya masoko wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya wamesema hawatopiga kura ya maoni
ya rasim ya katiba na kwa kuipigia kura
ccm kwa kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa masoko ulioanza kutekelezwa tangu
mwaka 2012 mpaka sasa mwaka 2015 haujakamilika.
Akiongea kwa
niaba ya wananchi diwani wa kata ya
kisiba bwana Samweli Mwakyusa kupitia
chama cha Mapinduzi amesema kwamba mradi
huo wa maji umeshusha hadhi ya chama cha
CCM kwa kuwa mradiwa maji umegubikwa na
utekelezaji mbovu na siasa zinazopelekea viongozi wa serikali na chama kutokuwa
waaminifu katika kutekeleza mradi huo na mpaka sasa wananchi kukosa maji.
Wakiongea wananchi mbele ya kamati ya maji
kilimo na mifugo iliyongozwa na mwenyekiti wa kamati Prf. Peter Kusolwa kiwemo
mbunge wa Rungwe magharibi Prf. David Mwakyusa mzaliwa wa kata hiyo ya masoko ambako mradi wa maji unatekelezwa,
wananchi wanashangaa kuona hata mbunge
wao hajawasaidia huku mkuu wa wilaya Crispin Meela akifanya ziara nyingi zisizo
na mafanikio katika mradi huo wa masoko .
Kamati ya Bunge ya maji kilimo na mifugo
ikiongozwa na mwenye kiti wa kamati prf.
Peter kusolwa na kuongozana na mbunge wa
Rungwe magharibi na kupokelewa na
mkuu wa wilaya, makamu wa halmashauri ya
Rungwe na busokelo na viongozi wa maji mkoa wa Mbeya na Tukuyu. imetembelea na kukagua miradi ya maji
wirayani Rungwe, miradi iliyotembelewa ni mradi wa kijiji cha itete na Kapugi
na mradi wa masoko.
Kabla ya
kukagua miradi hiyo mkuu wa wilaya alikabidhi ripoti za miradi hiyo na kuelezea
changamoto walizokumbana nazo kuwa ni kukosa wataaram wa maji, na madeni ambayo
yamepelekea kutomalizika kwa baadhi ya miradi. Hivyo alishauri serikali
kuanzisha wakara wa miradi ya maji vijijini kwani hii itawasaidia kupambana na
changamoto zinazowakabiri na ameitaka
wizara ya maji kuiga mbinu zinazofanywa na wizara ya miundo mbinu ili
kukamilisha miradi mikubwa ambayo haijakamilika.
Nae makamu
mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe diwani Ezekiel mwakota amesema kwamba
tatizo ni mtiririko wa fedha na ndio chanzo cha kutomalizika kwa miradi
mbalimbali. Na mradi uliokwama ni mradi wa masoko na ni kutokana na kukosa fedha za kuendelezea
mradi huo.
Wakazi wa
kijiji cha Itete na Kapugi wameipongeza serikari kwa kufanikisha mradi wa maji wa Kapugi na Itete na wameomba kuongezewa
mpira utakoakuwa unatoa maji kutoka chanzo kwenda kijiji cha Itete na Kapugi kwani bomba la mpira lililopopo linatumika na vijiji vitatu kikiwemo kijiji cha kyimo na halmashauri
tayari inampango wa kutoa mpira wa nchi tatu utakao peleka maji katika vijij vilivyoomba bomba hilo.
Kamati ya
maji kilimo na ufugaji imedai
kushughurikia matatizo hayo na kuwashauri wananchi kuunda kamati ya maji itakayosimamia miradi hiyo na kutunza
mazingira ili kutunza vyanzo vya
maji kwani vitawakomboa wasitembee
umbali mrefu wakitafuta maji na
wamewaasa kuchemsha maji ya kunywa kuepukana
magonjwa ya matumbo.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment