Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoliakizungumza na vyombo vya habari alipokuwa akitangaza Bar zilizotinga fainali ya Safari lager nyama choma. |
Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pichani. |
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli |
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza
bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano lauchomaji
nyama Mkoani Mbeya lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Hoteli ya Mikuyu, Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini,
Abubakari Masoli alisema Bar zilizofanikiwa kutinga fainali zimepatikana
kutokana na kura zilizopigwa na wateja wao.
Masoli alizitaja bar zilizoifanikiwa
kuingia fainali kuwa ni pamoja na Karembo Bar iliyoko Sokomatola,New City Pub
iliyopo Mwanjelwa,Tumaini Bar iliyopo Ilomba,Samaki Samaki Bar iliyopo Forest
ya zamani na Nebana Bar iliyopo Soweto jijini Mbeya.
Alisema fainali za mashindano ya
Safari Nyama Choma mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Chuo
cha Uhasibu (TIA) jijini Mbeya Februari 28,kuanzia saa mbili asubuhi na
kuendelea zikisindikizwa na Bendi ya TOT, na burudani zingine nyingi pamoja na zawadi
kemkem kutoka Safari Lager.
Alisema shindano hili hufanyika kila mwaka,ambapo kwa mwaka huu linafanyika kwa mara ya nane
mfululizo huku yakizinduliwa katika Mkoa
wa Mbeya na kufuatiwa na mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na mwisho Dar es
Salaam.
Aliongeza kuwa tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hilo limekuwa na
mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager
kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na
ushindi katika mkoa waliopo.
“Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa
watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango
bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama
katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha
katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma”alisema
Masoli na kuongeza.
“Tumezingatia maombi ya washiriki wa mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina
inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote
zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka
ya nyuma”.
Alisema washiriki watapimwa ujuzi wao katika
kutayarisha nyama choma za aina tatu ambazo ni nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya
kuku.
Alizitaja zawadi
watakazopata washindi walioingia katika fainali na kuibuka na ushindi kuwa ni
Mshindi wa kwanza ambaye ni Bingwa wa Mkoa atapata shilingi 1,000 000/=, Mshindi wa pili shilingi 800,000/=,Mshindi wa tatu
shilingi 600,000/=, mshindi wa nne 400,000/= na mshindi wa tano 200,000/=.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment