Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro
akizungumza na wananchi wa Chunya waliofika katika uzinduzi wa zoezi la
kusambaza nakala za katiba mpya inayopendekezwa kwa wananchi.
|
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro akiwasomea wananchi wake moja ya vipengere vilivyomo ndani ya Katiba inayopendekezwa. |
Mkurugenzi wa Halmashauri yaWilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, akitoa taarifa juu ya nakala zitakazosambazwa kwa wananchi wa Wilaya ya Chunya |
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro,
akiwagawia baadhi ya wananchi nakala za Katiba inayopendekezwa.
|
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kushuhudia
zoezi la kuzindua ugawaji wa Katiba wakifuatilia kwa makini.
|
Moja ya nakala za Katiba mpya inayopendekezwa.
|
HALMASHAURI ya Wilaya ya Chunya imeanza zoezi la
kuzisambaza nakala za Katiba mpya inayopendekezwa kwa Wananchi wake ili waweze
kuisoma na hatimaye kuipigia kura Aprili 30, mwaka huu.
Akizungumza na wananchi katika hafla ya kuzindua
zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro, iliyofanyika kwenye
stendi ya mabasi, alisema Wilaya imepokea nakala 10200 ambazo zitasambazwa
katika kata zote 34 ambapo kila Kata itapata nakala 380 kwa ajili ya
kuwasambazia Wananchi.
Kinawiro aliwataka Maafisa Watendaji wa Vijiji
na Kata kuhakikisha nakala hizo zinasambazwa kwa wakati katika maeneo yote
yanayohusika ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kuisoma kabla muda wa
kuipigia kura haujafika.
Alisema kunakuwa na tabia kwa baadhi ya
Watendaji wasio waaminifu ambao watataka kutumia urasimi wakati wa ugawaji wa
katiba pendekezwa jambo litakalochangia wananchi wengi kuzikosa ikiwa ni pamoja
na wao kukaa nazo maofisini na wengine kujaribu kuuza, jambo alilosema
halijakubalika na atakayebainika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa ili nakala
hizo za Katiba ziweze kuwafikia wananchi wengi na kwa wakati ni bora zoezi hilo
likafanyika kwa siku nne huku sekta mbali mbali na makundi maalumu yakipewa
kipaumbele zikiwemo idara za Serikali, Maktaba, ofisi za Vijiji na Kata na
Mashuleni.
Alisema kwa wazazi ambao hawajui kusoma na
wanapenda kusomewa ni bora Nakala hizo pia zikawafikia Wanafunzi ambao wataweza
kuwa msaada kwa hao watu baada ya wao kuzisoma na kuweza kuwasaidia
kuwaelimisha pale ambapo wataona kuna umuhimu wa kuelezwa.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, alisema Nakala za Katiba
hizo zimegawiwa kulingana na uhitaji na kuongeza kuwa kutokana na ukubwa wa
Wilaya na mchanganyiko wa watu waliopo idadi hiyo haitoshi kuwafikia wote.
Alisema kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2012 Wilaya
ya Chunya ina watu zaidi ya laki 3 ambao ni mchanganyiko wa wakulima, wafugaji,
wachimba madini, viongozi wa dini mbali mbali, watumishi wa taasisi za serikali
na taasisi binafsi ambazo zote zinapaswa kupewa kipaumbele cha kupata nakala za
Katiba inayopendekezwa.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment