WADAU
wa Sanaa mkoani Mbeya wameishauri Serikali kuweka sheria kali ili kudhibiti
kazi za wasanii kuuzwa kiholela madukani bila kuwepo kwa taarifa za wahusika
ambao ndiyo wenye kazi.
Aidha
wameshauri kuwa maduka yanayouza kazi za sanaa bila kuwa na vibali maalumu
kutoka Basata pamoja na wezi wa kazi za wasanii adhabu iongezwe kuwa kali zaidi
jambo litakalosaidia kukua kwa uchumi wa msanii mmoja mmoja pamoja na pato la
Taifa.
Hayo
yalibainishwa jana na Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam
Mtunguja, Protas Mpogole, katika hafla iliyoandaliwa na Chama cha Sanaa
Jiji la Mbeya(CHASAMBE)kwa ajili ya kuwatambulisha walezi wapya wa Chama hicho
iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya.
Mpogole
alisema pamoja na Chama hicho kuwaomba kuwa walezi bado ni jukumu la Serikali
kuhakikisha kazi za sanaa zinaimarishwa hususani katika fani za michezo na
utamaduni ili kukuza uchumi wa Nchi na msanii mmoja mmoja.
Alisema
kazi za sanaa zinadharauriwa sana na kuibiwa kutokana na baadhi ya wananchi
kutokuwa na utamaduni wa kuthamini shughuli zingine za michezo zaidi ya mpira
wa miguu jambo linalochangia Serikali kuongeza juhudi za maksudi ili kuinua
kazi za utamaduni.
Kwa
upande wake Kaimu Afisa Elimu Jiji la Mbeya, Kastor Ngonyani aliyemwakilisha
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Musa Zungiza katika hafla hiyo alisema Halmashauri
ya Jiji la Mbeya linakubali kuwa mlezi wa Chama hicho kutokana na umuhimu wake
katika kukuza ukuaji wa Halmashauri.
Ngonyani
alisema kutokana na umuhimu wa sanaa katika kutoa ujumbe mbali mbali kwa jamii
Halmashauri inavyo vitengo viwili ambavyo ni Idara ya Michezo pamoja na idara
ya utamaduni ili kuhakikisha shughuli zote zinazohusu sanaa zinaimarika.
Alisema
tangu awali kazi za sanaa ni chombo ambacho kilikuwa kikitumika katika
kufikisha ujumbe wowote katika jamii tofauti na michezo mingine kama mpira wa
miguu ambapo kupitia uigizaji ujumbe humfikia mlengwa moja kwa moja.
Naye
Katibu wa Chasambe, Ramadhan Ramadhan alisema tangu kuanzishwa kwa chama hicho
mwaka 2002 kimekuwa na mlezi mmoja ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbozi, Edna Mwaigomole hivyo kuona umuhimu wa kumuongezea nguvu kwa
kuteua walezi wapya.
Aliwataja
walezi wapya ambao kwa pamoja walikubali kuwa walezi wa Chama hicho kuwa ni
pamoja na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mbeya Jiji(OCD)Julius Mjengi, Mkurugenzi
wa Jiji la Mbeya Musa Zungiza, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariamu Mtunguja na
Mwenyekiti wa wamiliki wa Mahoteli Mkoa wa Mbeya, Jeremiah
Mahenge(Vamponji).
Aliwataja
wengine kuwa ni mfanyabiashara maarufu jijini Mbeya, James Mwampondele ambaye
pia ni Mkurugenzi wa AJIM Enterprises ltd,ambao wataungana na Mlezi wa Aawali
Edna Mwaigomole ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment