Merowe Dam wakati wa ujenzi Sudan
|
Mhe. Prof. Mwandosya akipata maelezo kutoka
kwa Wataalamu wa Merowe Dam Electricity Company
|
Mhe. Prof. Mwandosya alipata nafasi ya
kuongea na waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake
|
Mhe. Prof. Mwandosya alipata nafasi ya
kuongea na waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake
|
Picha ya pamoja kati ya Ujumbe wa Mhe. Prof. Mwandosya na Uongozi wa Merowe Dam Electricity Company |
Prof. Mwandosya akipata maelezo ya mitambo
ya kufuatilia uzalishaji umeme inavyofanya kazi
|
Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini
Sudan jana tarehe 15 Januari, alitembelea moja ya miradi mikubwa ya kuzalisha
umeme kwa kutumia mabwawa ambao unaendeshwa na Kampuni ya Merowe Dam
Electricity Company.
Mradi huu ambao uko Kaskazini mwa Nchi ya Sudan
umejengwa kwa gharama ya USD 2.0
millioni ambapo Serikali ya Sudan imechangia 30% na zilizobaki ilikuwa misaada
na mikopo kutoka kwa wafadhili wanje.
Mradi umejengwa kando kando ya Mto Nile
na una uwezo wa kuzalisha 1,250 megawati ambayo ni inachangia 60% hadi 70% ya
mahitaji ya nishati ya umeme nchini Sudan.
No comments:
Post a Comment