Katibu
wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo, Neema Stantoni, akiwa pamoja na mmoja
wa wafanyakazi wa mamlaka katika sherehe hizo.
MAMLAKA
ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya(Mbeya Uwsa) imesema inajivunia
mafanikio ya kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa utendaji wa Mamlaka za maji
Kitaifa na nafasi ya pili kwa utekelezaji wa shughuli za Maji taka na usafi wa
mazingira.
Hayo
yalibainishwa na Wafanyakazi wa Mbeya Uwsa katika risala yao mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe
ya kuuaga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka 2015 iliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini hapa.
Walisema
matokeo hayo yametokana na tahmini iliyofanywa na EWURA katika kupima utendaji
kazi wa Mamlaka zote kitaifa kwa mwaka uliopita hivyo kuonesha Mamlaka ya Maji
safi na usafi wa Mazingira Mbeya kushika nafasi ya pili kwa utendaji wa jumla
na nafasi ya pili kwa usafi wa mazingira.
Walisema
matokeo ya tathmini hiyo yanatoa hamasa ya kufanya vizuri katika mwaka 2015 na
lengo likiwa ni kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya jumla na
utekelezaji wa shughuli za mazingira.
Waliongeza
kuwa Silaha kubwa ya mafanikio hayo ni mpango uliopo wa matokeo makubwa
sasa(BRN) ulioanza Juni 2014 hadi Julai 2018 ambapo Mamlaka hiyo imepata
mafanikio katika utekelezaji wa mambo mbali mbali kwa mwaka 2014 ukilinganisha
na kipindi cha mwaka 2001 ilipokuwa ikianzishwa.
Waliyataja
mafanikio hayo kuwa ni ongezeko la wateja wa maji safi kutoka 9168 mwaka
2001/2002 hadi wateja 40709 mwaka 2014/2015, urefu wa mabomba ya kusafirisha na
kusambazia maji kutoka kilomita 108 hadi 710, wateja wa mati taka kutoka 42 hadi
1466 na jumla ya dira zilizofungwa kutoka 1931 hadi 40709.
Waliongeza
kuwa uwiano wa wateja wenye dira umeongezeka kutoka asilimia 21.06 hadi
asilimia 98.5, kupungua kwa upotevu wa maji kutoka asilimia 43 hadi asilimia
30.2, kuongezeka kwa uwezo wa kuzalisha maji kwa siku kutoka 18700 mita za
ujazo hadi mita za ujazo 51000, kiwango cha huduma kutoka asilimia 69 hadi
asilimia 95 na kuongezeka kwa muda wa upatikanaji wa maji kutoka masaa 14 hadi
masaa 23.1.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa bodi ya Maji safi na Usafi wa
Mazingira Mbeya, Jaji Atuganile Ngwala, alisema mafanikio yaliyopatikana mwaka
2014 yametokana na ushirikiano baina ya uongozi wa bodi na watumishi wa mamlaka
na wateja wao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alitoa wito kwa Wafanyakazi
wa Mamlaka hiyo kuacha kubweteka na mafaniko waliyoyapata bali kuongeza kasi ya
kuzikabili changamoto zilizojitokeza katika kipindi hicho.
Aliwataka
wafanyakazi kuacha kuishi maisha ya juu hali itakayosababisha kuwa na tama na
kuwapelekea kutukuwa waaminifu katika mali za mamlaka na kuwasihi kuishi maisha
kulingana na uwezo na vipato vyao.
Aliongeza
kuwa timu za ukaguzi za Mamlaka hiyo hasipaswi kukaa ofisini bali zizunguke
jambo litakalosaidia kupatikana kwa mtandao wa watu wanaojiunganishia maji,
wezi wa maji na wanaoiba Dira za maji.
Kandoro
alisema ni jukumu la kila mwananchi kushirikiana katika utunzaji wa mazingira,
kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kuacha tabia ya kulima , kuchunga mifugo, kuchoma
moto kwenye vyanzo vya maji hali itakayochangia uharibifu wa mazingira na
kukauka kwa vyanzo vya maji.
Alisema
takwimu zinaonesha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita jumla ya vyanzo vya
maji 40 vimekauka kutokana na kuharibu mazingira na kufanya shughuli za
kibinadamu karibu na vyanzo vya maji bila kuchukua tahadhari zozote.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment