Sehemu ya barabara ambayo imekamilika baada ya kumwagwa kifusi na kushindiliwa tayari kwa kuanza kutumika.
UONGOZI wa Halmashauri ya Jiji
la Mbeya umelazimika kutoa ufafanuzi wa sintofahamu kuhusu ukarabati wa
barabara ya Iganzo- Kabwe kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi.
Baadhi ya Wakazi wa Isanga
walitoa malalamiko yako kwa vyombo vya habari wakilalamikia hatua
zilizocghukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuamua kukarabatio
Barabara ya Iganzo- Kabwe kwa kufukia vifusi vya mawe juu ya Lami huku
wakihofia mvua zinazonyesha kuweza kuharibu.
Kutokana na malalamiko hayo na
kuripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari baada ya uongozi wa Jiji
kushindwa kujitokeza ili kuyatolea ufafanuzi ndipo Mhandisi wa Jiji la Mbeya,
Laynas Sanya, akalazimika kufika eneo la mradi na kuzungumza na vyombo vya
habari.
Mhandisi Sanya alisema
ukarabati unaofanyika katika barabara hiyo ni kwa ajili ya kupitika katika
kipindi kifupi wakati Uongozi wa Jiji ukijipanga kufanya ukarabati mkubwa hivyo
kulazimika kuziba kwenye sehemu zilizokuwa zimechimbika sana huku sehemu nzuri
zikirukwa.
Alisema baada ya kifusi
kumwagwa Greda hupita na kuvuruga sehemu ya Lami ilichini ikichanganya na
kifusi kisha kushindiliwa vizuri hali itakayosaidia njia hiyo kupitika kirahisi
na kurahisisha masuala ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.
Aliongeza kuwa mbali na
Halmashauri ya Jiji la Mbeya kukosa fedha za kujenga upya barabara hiyo pia
ikio kwenye mazungumzo ya kuifanya Barabara hiyo kupandishwa hadhi na kuwa ya
Mkoa.
Akizungumzia kuhusu vifaa na
Ukandarasi alisema kazi hiyo inafanywa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa
kufuata kanuni za manunuzi ya umma isipokuwa Vifaa vilikosekana na kulazimu
kukodi kwa Mkandarasi wa kampuni ya China Communications Contractor Company
Ltd(CCCC) na kufanya jumla ya gharama zote kufikia shilingi Milioni 37.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment