Afisa Umwagiliaji wa Skimu ya Igomelo,
Ramadhani Makombe akielezea namna wakulima wanavyonufaika na Skimu hiyo
sambamba na utunzaji wa maji.
|
Afisa Umwagiliaji wa Halmashauri ya Jiji
la Mbeya, Mwakibete Kasilati akitoa muongozo juu ya lengo la ziara ya wakulima
na Maafisa kilimo wa Jiji la Mbeya katika Skimu ya Igomelo.
|
Mjumbe wa bodi ya Skimu ya umwagiliaji
ya Igomelo, Zainabu Mgeni akisoma taarifa kwa wakulima na maafisa kilimo kutoka
Jiji la Mbeya waliowatembelea.
|
Baadhi ya Wakulima na maafisa kilimo
kutoka Jiji la Mbeya wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wenyeji wao
viongozi wa Skimu ya Igomelo.
|
Afisa kilimo kutoka Iganjo jijini
Mbeya, Elizabeth Mushi akiuliza maswali juu ya changamoto ya soko kwa wakulima
wa Skimu ya Umwagiliaji ya Igomelo.
|
Katibu wa Ushirika wa Skimu ya Igomelo,
Japhet Mvukali akifafanua jambo.
|
Maafisa Kilimo kutoka Jiji la Mbeya
wakichukua dondoo mbali mbali zilizobandikwa katika mbao zilizomo kwenye ofisi
za ushirika wa skimu ya Igomelo.
|
Mwekiti wa Skimu ya Igomelo, Nelson
Vicent akiwaonesha baadhi ya maelezo yaliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo
wakulima na maafisa kilimo kutoka jijini Mbeya.
|
Afisa Umwagiliaji wa Skimu ya Igomelo,
Ramadhani Makombe, akitoa maelezo kwa Wakulima na maafisa kilimo kutoka Jijini
Mbeya.
|
Mkulima wa Nyanya katika shamba la
Skimu ya Igomelo, Devotha Katawa akitoa maelezo juu ya maendeleo ya mazao
katika shamba lake.
|
wakulima na Maafisa Kilimo kutoka Jiji
la Mbeya wakiwa shambani wakijionea namna mazao yanavyostawi kutokana na kilimo
cha umwagiliaji.
|
Afisa Kilimo jiji la Mbeya, Advera
Kahitwa akiwaongoza Wakulima na maafisa Kilimo kupata maelezo mbali mbali juu
ya kilimo cha umwagiliaji kutoka kwa Mkulima wa Skimu ya Igomelo Devota Katawa.
|
Wakulima na Maafisa Kilimo kutoka Jiji
la Mbeya wakipata maelezo katika shamba la Nyanya.
|
Baadhi ya mabango yakionesha hatua mbali
mbali zinazochukuliwa na uongozi wa Skimu ya Igomelo kwa wakulima wanaokiuka
taratibu za uendeshaji wa Skimu.
|
Wakulima na maafisa kilimo wa
Halmashauri ya Jiji la Mbeya walipata fursa pia ya kutembelea Banio kubwa la Maji
katika Mto Mbarali na kupeleka maji katika Skimu ya Igomelo.
|
Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la
Mbeya, Advera Kahitwa akiwaonesha wakulima na Maafisa Kilimo jiji la Mbeya
namna matunda ya pilipili hoho yalivyo makubwa yaliyovunwa tayari kupelekwa
sokoni.
|
Picha ya Pamoja katika ya Maafisa Kilimo
Jiji la Mbeya na Wenyeji wao ambao ni viongozi wa Skimu ya Igomelo.
|
Picha za pamoja za wakulima kutoka Skimu
za Iganjo, Imbega na Ikanga wakiwa wamepiga na Maafisa Kilimo wa Jiji la Mbeya.
|
picha ya pamoja ya Wakulima na maafisa
kilimo Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na viongozi wa Skimu ya umwagiliaji
ya Igomeli baada ya kukamilisha kwa ziara yao ya kimafunzo.
|
Mojaya Maghala ya kuhifadhia vitunguu
vya Wakulima wa Skimu ya umwagiliaji ya Igomelo.
|
Mmoja wa Wakulima wa Vitunguu katika
Skimu ya Umwagiliaji ya Igomelo wilayani Mbarali akichukua zao hilo kutoka
katika ghala alilokuwa amehifadhia tayari kwa kupeleka sokoni.
|
WAKULIMA
nchini wametakiwa kuwawabunifu katika kuendesha kilimo chenye tija na sio
kubweteka majumbaniwakisubiri wataalamu ili waweze kuwapa mbinu ili hali
Serikali inakabiliwa naupungufu wa maafisa kilimo.
Wito
huo ulitolewa na Afisa umwagiliaji wa Skimu ya Igomeloiliyopo wilayani
Mbarali Mkoa wa Mbeya, Ramadhan Makombe, alipokuwa akitoamaelekezo kwa Wakulima
15 na Maafisa Kilimo 18 kutoka Halmashauri ya Jiji laMbeya waliofanya ziara ya
kimafunzo katika Skimu hiyo ambayo ni skimu ya nnekwa ubora kitaifa.
Makombe
alisema Mafanikio yaSkimu ya Igomelo yametokana na wakulima kutozubaa kusubiri
maafisa Kilimo ilikuwapa maelekezo mbali mbali bali wao wenyewe wamekuwa
wakifanya jitihada mbalimbali ili kuongeza uzalishaji katika Skimu zao ambapo
hulazimika kuwatafutawataalam pindi wanapokwama
.
Alisema Skimu hiyo yenyewakulima 294 wakiwemo wanawake 65 na wanaume 179 katika
Shamba lenye ukubwa waHekta 312 ni vigumu kwa wataalam kuweza kuwafikia wote
kwa wakati mmoja jamboambalo linaweza kukwamisha uzalishaji wa mazao.
Naye
Mwenyekiti wa Ushirika waIgomelo unaosimamia Skimu hiyo, Nelson Vicent, alisema
wakulima katika Skimuhiyo wamenufaika na mafunzo mbali mbali wanayoyapata
kutoka kwa wataalam jambolililopelekea kila mtu kuwa mtaalam wa kilimo na
kujikita katika kilimo chenyetija.
Aliongeza
kuwa uwepo wa Skimuhiyo inayotegemea maji kutoka Mto Mbarali hivyo kuwezesha
kulima kilimo chaumwagiliaji kwa kipindi chote cha Mwaka imesaidia kupunguza changamoto
yaVijana kukimbilia mjini na kuacha shughuli za kilimo vijijini na kufanya
kijijicha Igomelo kutokimbiwa na Vijana.
Alisema
tangu kuanzakujihusisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu hiyo mwaka 1998
kumekuwa nautofauti wa uzalishaji wa mazao wanayolima ambapo alisema uzalishaji
wa mahindiumeongezeka kutoka Tani 1.5 kwa Hekta hadi tani 3.7, Mpunga kutoka
tani 2 haditani 4, Vitunguu kutoka tani 13 hadi tani 26 na Nyanya kutoka tani 5
hadi tani35.
Kwa
upande wake kiongozi waMsafara wa Wakulima na Maafisa kilimo kutoka Jiji la
Mbeya, Afisa umwagiliajiwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mwakibete Kasilati,
alisema lengo la kufanyaziara hiyo ni kutaka Wakulima na maafisa kujifunza
namna ya uendeshaji wa skimu unavyofanywa.
Aliyataja
malengo mengine kuwani kujua namna ya utunzaji wa skimu hadi kupata mafanikio
na kuwa skimu ya nnekwa ubora kitaifa pamoja na namna walivyofanya kuimarisha
vikundi katika Skimuya Igomelo.
Kasilati
alisema katika Ziarahiyo ilihusisha wawakilishi wa Wakulima kutoka Skimu za
Iganjo, Ikanga naImbega zote za jijini Mbeya wapatao 15 na Maafisa kilimo 18
kutoka katika Kata zaHalmashauri za Jiji la Mbeya ambapo walipata nafasi
ya kuwauliza maswali mbalimbali viongozi wa Skimu ya Igomelo pamoja na
kutembelea eneo la Skimu.
Naye
Afisa Kilimo Jiji laMbeya, Advera Kahitwa alisema pamoja na Jiji la Mbeya
kuendelea kukua hivyokuwa na ufinyu wa ardhi ya kuendeshea kilimo bado kuna
ulazima wa kutengamaeneo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment