Picha ya pamoja ya wanafamilia wa NMB Mbeya
WAFANYAKAZI
wa Benki ya NMB Mbeya mjini wameungana na familia zao kusherehekea siku ya
Familia iliyofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Ifisi.
Akizungumza
katika sherehe hizo Meneja wa Kanda, Lecrisia Makiriye, alisema benki
inathamini mchango wa watumishi pamoja na familia zao ndiyo maana hutenga siku
moja kwa ajili ya kukutana.
Aidha
alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika maadili mema na
mazuri kwa kuwaepusha kujiingiza katika vitendo viovu ili siku moja waje kuwa
watumishi katika fani mbali mbali kwa manufaa ya taifa.
Meneja
huyo aliwaambia wanafamilia wa NMB kuwa Benki hiyo imekuwa kubwa kiasi kwamba
shughuli zake zimeongezeka na kufikia kuwa na matawi mengi zaidi kuliko benki
yoyote nchini pamoja na ATM zaidi ya 400 nchi nzima hivyo wanapaswa
kushirikiana.
Katika
Sherehe hizo Wanafamilia wa NMB walishiriki mazoezi ya viungo pamoja na michezo
mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu, kuvuta kamba, kukimbia
kwenye magunia na kukimbiza kuku pamoja na chemsa bongo kwa watoto.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment