Meza kuu katika maadhimisho ya Ukimwi duniani ikiongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni Askofu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo, yaliyoadhimishwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika viwanja vya Shule ya Msingi Mbata.
Naibu Meya na Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti Ukimwi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Chieforder Fungo akimuongoza Mgeni rasmi Askofu Alinikisa Cheyo kutembelea mabanda katika maadhimisho ya Ukimwi duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mbata.
Mgeni rasmi ambaye ni Askofu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo, akitembelea banda la Damu salama katika maadhimisho ya Ukimwi duniani yaliyoadhimishwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika viwanja vya Shule ya Msingi Mbata.
Mgeni rasmi pamoja na viongozi alioambatana nao wakiwa wameshika mishumaa kabla ya kuiwasha.
Mwenyekiti wa Mtandao wa wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(KONGA), Mzee Deogratius Kisunga, akimsaidia kuwasha mshumaa mgeni rasmi kama ishara ya kuwakumbuka waliofariki dunia na kutoa dira ya mwelekeo wapi tunakoelekea na tulikotoka.
Wageni mbali mbali wakiwa wameshika mishumaa katika kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiungana na wakazi wa Jiji la Mbeya katika maadhimisho ya Ukimwi duniani.
Alfred Sanga na Mkewe wakitoa ushuhuda baada ya kuishi na virusi kwa muda mrefu lakini wakafanikiwa kupata mtoto asiye na maambukizi na baadaye ikabainika mama kupona kabisa Ukimwi kutokana na kuzingatia matumizi sahihi ya ARV.
Wananchi mbali mbali wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti.
Baadhi ya vibanda katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbata vilivyokuwa vikitoa huduma ya ushauri nasaha na kupima virusi vya Ukimwi katika maadhimisho ya Ukimwi duniani.
Wananchi wakiwa kwenye maandamano wakielekea kwenye viwanja vya shule ya msingi Mbata katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.
Timu za Netball zikiendelea na mchezo katika maadhimisho hayo.
Kikundi cha Burudani cha Makhirikhiri cha Mbeya kikitoa Burudani kwa wageni mbali mbali.
Timu ya Mpira wa miguu ikiendelea na mchezo katika maadhimisho hayo.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment