MKUU
wa wilaya ya Mbeya Dk. Norman Sigallah King, juzi usiku aliwaongoza
wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye chakula cha hisani ya kuchangia ujenzi wa
njia za kupitishia wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Hafla
hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Beaco iliyopo Forest jijini Mbeya
ambapo lengo lilikuwa ni kukusanya Shilingi Milioni 150 ili kukamilisha ujenzi
wa Njia za kupitishia wagonjwa.
Akizungumza
na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya, Dk. Norman Sigallah,
aliwapongeza Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya sambamba na waanzilishi wa
wazo la kujenga njia hizo katika Hospilai hiyo.
Alisema
siku zote afya zinapaswa kupewa kipaumbele ili shughuli zingine zziweze
kufanikiwa vizuri ambapo pia alitoa wito kwa Wananchi wengine kujitokeza kutoa
michango yao ili kukamilisha ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi
za waanzilishi wa wazo hilo.
Awali
akimkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya Marafiki wa Hospitali ya
Mkoa wa Mbeya, Oleais Senga, alisema wazo la awali lilikuwa ni kukarabati paa
la Wadi ya akina mama lililokuwa likivuja ambapo baada ya kuchangishana wakaona
wasishie hapo bali wajenge na njia za kupitishia wagonjwa.
Alisema
mara ya kwanza walichangishana na kupata shilingi Milion 7 ambazo walitoa
shilingi milioni moja na kupeleka kukarabati Paa na fedha zingine zilisaidia
kuandaa harambee ambayo ilifanyika Mwezi Machi mwaka huu na kupata shilingi
Milioni 81ikiwa ni Ahadi na fedha taslimu.
Alisema
tangu hapo hatua mbali mbali zilianza kwa kuwapata wasanifu wa kuchora ramani
pamoja na Mkandarasi ambapo kazi ilianza bilakujali kiasi cha fedha
kilichopatikana.
Alisema
hadi sasa Njia ambazo zilipaswa kujengwa zinaurefu wa Mita 405 kati yake Mita
165 zimejengwa kwa kiwango cha sakafu na kuezekwa na mita 104 zikiwa
zimesakafiwa bila kuezekwa hivyo kubakiwa na mita 146 ambazo hazijaguswa
kabisa.
Alisema
hadi sasa kinatafutwa kiasi cha Shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kumalizia
ujenzi wa mita 146, kuezeka mita 104 na kujenza mitaro kwa ajili ya kupitishia
maji ya mvua.
Alisema
ujenzi huo unafanywa na Mkandarasi wa kampuni ya Inter Frempa Co.Ltd yenye
makao makuu jijini Mbeya pamoja na Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia(MUST)
waliojitolea kuchora ramani ya ujenzi huo bure bila malipo yoyote.
Alisema
kujitolea kwa watu hao kumepunguza baadhi ya gharama na kurahisisha ujenzi na
kutoa wito kwa wadau kujitoa kwa hali na mali ili ujenzi huo ukamilike kwa
wakati kupitia Mpesa 0762 321829 yenye jina la Marafiki Mkoa au
akaunti namba 0150067027600 CRDB jina Marafiki wa Hospitali ya Mkoa
wa Mbeya.
Hata
hivyo katika Chakula cha Hisani jumla ya shilingi Milioni 26,036,000
zilipatikana zikiwemo fedha taslimu shilingi Milioni 4,646,000 na Ahadi
shilingi Milioni 21,390,000/=.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment