Zaidi
ya nyumba 38 zimeezuliwa na upepo ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha
mwishoni mwa juma katika kijiji cha Mapogolo Kata ya Chokaa wilaya ya Chunya
Mkoani Mbeya.
Hayo
yamethibitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Deodatus Kinawiro alipowatembelea
wahanga akifuatana na Mkurugenzi wa Halmashauri Sophia Kumbuli ambapo
walitembelea wahanga na kuwapa pole.
Janga
hilo pia lileta athari kwa kanisa la EAGT ambalo liliezuliwa paa lote na
kusababisha mabati yaliyoezekwa hivi karibuni baadhi kuharibika vibaya hivyo
kutofaa kuezekewa tena.
Kwa
mujibu wa Taarifa ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapogolo Samwel Komba iliyosomwa
na Mtendaji wa Kijiji Linus Mkumbwa imesema kuwa hakuna vifo wala madhara
yoyote kwa binadamu ingawa baadhi ya vyakula vimeharibika na wahanga
wamehifadhiwa na ndugu na marafiki.
Kutokana
na baadhi ya familia kuwa na hali ngumu ya maisha na wengi wao kuwa ni wazee
Mkuu wa Wilaya aliongoza Harambee ya papo hapo ambapo jumla ya shilingi laki
nane na elfu ishirini zilipatikana kutoka kwa viongozi walioambatana na Mkuu wa
Wilaya na wananchi waliofika kumsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Hata
hivyo Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa wananchi kuwa fedha hizo zitumike kununua
mahitaji muhimu kama misumari,mbao na mabati kwa watu wasio na uwezo pia mafundi
wajitolee kusaidia kuezeka ili wahanga wapate hifadhi.
Aidha
ametoa agizo kwa Mhandisi wa Ujenzi Nuru Ndelwa kusaidia kusimamia ukarabati wa
nyumba hizo kwani nyingi ya nyumba zilizoezuliwa zilikuwa haziko kwenye kiwango
hali ilyosababisha kuezuliwa kutokana na mabati kupigwa bila mtambaa panya.
Kinawiro ametoa wito kwa wadau
mbalimbali kusaidia michango ya hali na mali wananchi hao na kwamba suala hilo
lipo ndani ya uwezo wao na Wilaya kwa ujumla kwani kutoa ni moyo wala si
utajiri.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
poleni sana ndugu zetu. Jengeni nyumba bora na imara kustahimili mvua na upepo.
Post a Comment