Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla akizindua kampeni ya Chanjo jijini Mbeya hivi karibuni |
Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa
Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro, wakati wa uzinduzi wa Chanjo hiyo
iliyofanyika katika kituo cha Afya Ruanda kilichopo Mwanjelwa jijini hapa
ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla.
Dk. Lazaro alisema kampeni ya chanjo
hizo ni ya kitaifa ambapo zoezi hilo litadumu kwa muda wa wiki moja na kuzitaja
aina za Chanjo hizo kuwa ni pamoja na Surua Rubella itakayowalenga watoto wa
miezi 9 hadi miezi 59 wapatao 171,862, chanjo nyingine ni matone ya vitamin A
itakayowalenga watoto kuanzia miezi 6 hadi 59 wapatao 62,772.
Alizitaja aina zingine za Chanjo kuwa ni
dawa ya minyoo ya Mabendazole kwa watoto wote wenye umri wa miezi 12 hadi miezi
59 wapatao 50580 na dawa ya Invermectin na Albendazole zinazokinga Usubi,
Minyoo ya tumbo matende na mabusha kwa wenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea
wapatao 345110.
Aliongeza kuwa ili zoezi hilo lifanikiwe
Halmashauri imeandaa vituo vingi vitakavyoendesha kampeni ya Chanjo na kuligawa
katika aina mbili ambazo alizitaja kuwa ni vituo vya kudumu na vituo vya muda
ambavyo watalaamu watakuwa wakihama hama kufuata watu walipo.
Alisema vituo hivyo vitakuwa 79 vikiwa
na jumla ya watumishi 553 ambavyo alivitaja kuwa ni pamoja na Kliniki za huduma
za afya ya uzazi na Mtoto, shule zote za msingi na Sekondari,Stendi za mabasi,
Stesheni za Treni na sehemu yoyote itakayoonekana kufikika kiurahisi na jamii
na sehemu yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya mkusanyiko wa watu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,
Dk. Norman Sigalla, aliwakemea wananchi wengi wanapotoshwa na imani potofu
kuhusiana na chanjo hizo kwamba zinapunguza na kusababisha matatizo kwenye
upande wa uzazi.
Alisema chanjo ni muhimu kwa watoto kwa
sababu itamsaidia baadaye kutopata magonjwa ambayo hayatibiki kirahisi jambo
litakalowagharimu wazazi na kuishia kulaumiana baada ya matatizo kutokea dhidi
ya watoto wao.
Alisema utafiti unaonesha idadi kubwa ya
watu wanaopata magonjwa ukubwani, kupoteza uwezo wa kufikiri na kuwa
wasahaulifu wanakuwa hawakupata chanjo wakiwa watoto.
Alisema baadhi ya magonjwa kama Matende,
mabusha, usubi na minyoo ya tumbo yanadhibitiwa kupitia chanjo pekee na kwamba
kuyatibu baada ya kutokea ni vigumu kutokana na mwili kukosa chanjo tangu
mwanzo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment