Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 3, 2014

HOT NEWS: KESI YA MCHUNGAJI KUISHI NA MKE WA MTU YAENDELEA,AKAMATWA TENA NA KESI YA KUTELEKEZA MKE NA WATOTO



Kesi ya madai inayomkabili Mchungaji Justin Israel Mwakifuna(36) wa Kanisa la Jeshi la Bwana imeendelea kusikilizwa katika mahakama ya Mwanzo Iyunga Jijini Mbeya
.
Kesi hiyo ilifunguliwa na William Mwasubila dhidi ya Mchungaji huyo akidai kuishi kinyumba na mke wake aliyefahamika kwa jina la Helena Mkea(20)kinyume cha sheria tangu mwezi mei mwaka huu katika eneo la Nzovwe Jijini Mbeya.
Mwasubila na mkewe ni waumini wa Kanisa hilo ambapo walifika Kanisani hapo kufanyiwa maombi kutokana na mkewe kusumbuliwa na mapepo kwa muda mrefu bila mafanikio.

Hata hivyo baada ya kupatiwa huduma ya maombi mchungaji alianza mahusiano ya kimapenzi na muumini wake hali iliyopelekea mkewe mchungaji aliyefahamika kwa jina la Lea Martin(30) kuondoka nyumbani baada ya mchungaji kuzididisha vitimbi.
Upande wa madai ulileta mashahidi ulileta mashahidi wawili akiwa Baba mzazi wa mchungaji na mkewe mchungaji mwakifuna.

Baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Nasoni Mwakifuna(79)mkazi wa Forest ya zamani aliiambia mahakama mbele ya mheshimiwa Nuru Lyimo kwamba mwanawe ni mtoto wa tatu katika familia yake na kwamba alifunga ndoa halali ya Kikristo katika Kanisa la Restoration Bible Church lililoko Forest mpya Jijini Mbeya mwaka 2002.
Aidha alishangaa siku za hivi karibuni baada ya kupoka malalamiko kutoka kwa mke wa Jaliyedai mume wake ana mahusiano ya kimapenzi na Helena ambaye ni mke wa muumini wake baada ya kuzikuta sms kweye simu ya mumewe ndipo alitoa taarifa ambapo walisuluhishwa.

Baada ya suluhu hiyo bado Mchungaji aliendelea mahusiano na muumini wake hali iliyomfanya kuamua kwenda kupumzika kwa wazai wake eneo la Forest aikwa na watoto watatu wa kike wawili wakiwa wanafunzi wa shule ya msingi Mapambano darasa la sita.
Mahakama ilangua kicheko pale ambapo Baba mzazi alipomwambia ammweleze Mungu gani anayemwabudu kwa kuishi na mke wa mtu huke akinukuu maandiko kutoka kitabu cha Luka 16:18maneno yakisema anayezini na mke wa mtu afanya uasi huku mwanae akipinga akitumia kitabu cha aagano la kale.

Shahidi wa tatu alikuwa ni mke wa Mchungaji ambaye aliiambia mahakama kuwa yeye ni mke halali waliyefunga ndoa ya kikristo na Justin mwaka 2002 na kujaliwa kupata watoto watatu wa kike wakwanza akiitwa Eliza wa pili Hana na watatu Debora.

Aliiambia mahakama baada ya kupata taarifa za mahusiano ya kimapenzi na Helena alifanya uchunguzi hadi kubaini sms walizokuwa wakitumiana na kupata taarrifa kuwa mchungaji alikuwa alifanya mapenzi Kanisani na muumini wake ambapo alitoa taarifa kwa wazai wa pande mbili lakini hawakufikia muaafaka kutokana na baba yake mzazi kuugua na kupoteza maisha.

Baada ya ushahidi wa mke wa mchungaji kesi iliahirishwa hadi sepemba 5 mwaka huu upande wa madai utakapoleta mashahidi wengine.

Ajijiandaa kutoka Mchungaji alikamatwa na kufunguliwa mashitaka mbele ya Hakimu Shughuli Mwampashe akikabiliwa na kosa la kutelekeza mke na watoto watatu kinyume cha sheria kifungu cha 167 sura ya 16 iliofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka.

Kesi hiyo imefunguliwa na Baba mzazi wa Justin Nasoni Mwakifuna ambapo shahidi wa kwanza aliyetoa ushahidi ni mke wa Justin ambaye aliiambia mahakama kuwa ametelekezwa na mumewe kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila mahitaji muhimu.


Kesi itaendelea kusikilizwa septemba 4 mwaka huu upande wa mashitaka utakapoleta mashahidi wengine na mshitakiwa amedhaminiwa kwa dhamana ya maandishi ya shilingi laki tano kila mmoja.


Na Mwandishi wetu Mbeya

No comments: