Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 5, 2014

Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh Abbas Kandoro afungua mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya



 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mh. Abbas Kandoro  akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Mbaspo wakati akifungua rasmi mashindano ya Airtel Rising Stars.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mh. Abbas Kandoro  akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Mbozi wakati akifungua rasmi mashindano ya Airtel Rising Stars.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya 



Kandoro afagilia mashindano ya vijana.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amefungua rasmi mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya na kusisitiza umuhimu kwa wadau wote wa soka kutilia maanani programu za vijana. Ufunguzi huo ulifanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya juzi Jumatatu. 

“Hii ndio njia pekee ambayo inaweza kutuletea maendeelo ya soka na kuiwezesha nchi yetu kuondokana na matokeo mabaya katika mashindano mbali mbali ya kimataifa”, alisema. Aliishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kubuni programu hii ambayo imekuwa ikiwapa vijana fursa ya kuonyesha na kuviendeleza vipaji vyao.

Aliwataka vijana kucheza kwa kujituma na kuwataka wafahamu kwamba hatma ya mchezo wa soka kwa siku za usoni iko mikononi mwao “Miamba yote ya soka ambayo tunaihusudu na kuishabikia hivi leo imepata mafanikio hayo makubwa baada ya kuwekeza na kutilia manani soka la vijana na naamini kwamba kwa mwendo huu na sisi tutapata mafanikio ya kuridhisha. Ni suala la muda tu”, alisema.

Amewataka viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA) kuyatumia vizuri mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa na kuchagua vijana nyota watakaounda timu ya mkoa kushiriki kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 10 hadi 17.

Fainali za Taifa zitashirikisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Timu nyingine zitatoka Morogoro, Mwanza, Mbeya na Zanzibar. Alisema mbali na kutumika kubaini vipaji vya soka, programu ya Airtel Rising Stars pia inatoa fursa kwa vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwafanya kuwa na afya njema.

Kalenda ya mwaka ya Airtel Rising Stars inatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa mwezi huu ambapo zaidi ya nchi 20 za Afrika zitachuana kwenye mashindano ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika nchini Gabon. Katika kindumbwendumbwe hicho Tanzania itawakilishwa na timu za wavulana na wasichana zenye wachezaji 16 kila moja. Wawakilishi hao watachaguliwa wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa MREFA Juma Killa ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kubuni programu hii ili kutumika kama jukwaa linatotumika kubaini vipaji vya wanasoka chipukizi. Alisema kuwa mashindano ya Airtel Rising stars yameifanya kazi yao ya kutafuta vipaji vya soka kuwa rahisi zaidi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja wa Airtel Tanzania Kanda ya Mbeya Straton Mushi amewashukuru wadau wote wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili.

No comments: