Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 19, 2014

MADIWANI CHUNYA WAWAOMBEA WANANCHI WAO KONDOMU.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Kapala Chakupewa Makelele akifungua mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika jana wilayani hapo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,Charles Mwakalila akisoma ajenda za Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya, Sosthenes Mayoka, akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Chunya.
 Madiwani na wakuu wa idara wakifuatilia kwa makini Mkutano wa baraza la Madiwani wa Wilaya ya Chunya uliofanyika jana.

**********************************
 
KATIKA kuhakikisha gonjwa la Ukimwi halisambai kwa kasi miongoni mwa Wananchi, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameitaka Serikali kuongeza Kondomu katika maeneo ya mikusanyiko.
 
Madiwani hao walitoa rai hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, ambapo walisema katika maeneo ya Mfwenkenya, Lupa na Namsinde yana kiwango kikubwa cha maambukizi.
 
Walisema ili kunusuru hali hiyo ni bora Kondomu zikasambazwa za kutosha katika maeneo hayo ama kuwaruhusu wafanyabiashara kuuza kwa wingi katika maduka yao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu jinsi ya kutumia na kujikinga na maambukizi.
 
Waliongeza kuwa maeneo ya ya mikusanyiko ya watu ndiyo inatakiwa kupewa vipaumbele sana kutokana na kuwepo mchanganyiko wa watu wenye tabia tofauti pamoja na mabinti wanaofanya biashara za ngono.
 
Diwani wa kata ya Mbangara, Abrahamu Sambira, alisema hali ya maambukizi inatisha kutokana na mabinti kulazimisha kufanya ngono na wanaume kwa malipo ambapo hufikia hatua ya kuomba hata mahindi kwa mwanaume asiyekuwa na fedha.
 
“ Ndugu zangu hali ni mbaya mabinti wanalazimisha mapenzi ambapo wanakuuliza kuwa kama huna fedha lete hata mahindi hivyo kuifanya shughuli hiyo kama halali wakati ni hatari” alisisitiza Diwani huyo.
 

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dk. Sichalwe alisema suala la upatikanaji wa Kondomu ni kubwa kwa Wilaya nzima hivyo ataendelea kulifanyia kazi ili kunusuru hali hiyo.

Na Mbeya yetu

No comments: