VYOMBO vya habari vimeelezwa kuwa ndiyo
kichocheo kikubwa cha amani duniani kote hivyo vinapaswa kutoa taarifa zenye
kuhamasisha hali ya amani na utulivu katika jamii ya Tanzania.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigalla King ambaye alimwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro katika hafla ya kufungua mafunzo ya kituo cha
Redio cha Bomba kilichopo Jijini Mbeya yanayotolewa na Shirika la Utangazaji la
BBC.
Alisema kujengeka au kutokujenga kwa
amani katika jamii kunategemea vyombo vya habari jinsi vilivyotangazana hivyo
Wananchi kuhamasika kutokana na kile wanachokisikia na kuelezwa.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo
kutoka Shirika la Utangazaji la BBC la Uingereza, Pendael Omary, alisema lengo
la mafunzo hayo ni kuongeza weledi wa kazi ya habari kwa vituo vua Redio vya
Mikoani.
Alisema vyombo vya habari vinakazi ya
kubadilisha maisha ya watu kupitia vipindi mbali mbali vinavyotangazwa ambavyo
vinakuwa vimefanyiwa utafiti na kuwa na manufaa kwa jamii.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment